Wachibaji madini wadogo vicheko Serikali ikifuta kodi

Rais Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda mbalimbali ya wachimbaji wadogo wa madini kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Jumamosi Oktoba 21, 2023.
Muktasari:
- Ikiwa ni moja ya njia za kukuza sekta ya madini nchini, Serikali imefuta kodi ya ongezeko la thamani ya asilimia 18 (Vat), pamoja na kodi ya zuio ya asimilia tano kwa wachimba wadogo watakao uza madini katika masoko ya ndani amesema Rais Samia Suluhu Hassan.
Dar es Salaam. Ikiwa ni moja ya njia za kukuza sekta ya madini nchini, Serikali imefuta kodi ya ongezeko la thamani ya asilimia 18 (Vat), pamoja na kodi ya zuio ya asimilia tano kwa wachimba wadogo watakao uza madini katika masoko ya ndani amesema Rais Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 21, 2023, kwenye uzinduzi wa mitambo ya kuchorongea madini kwa wachimbaji wadogo na Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
“kwa sasa pia tumetoa punguzo la asilimia mbili ya mrabaha pamoja na kuondoa asilimia moja ya ada ya ukaguzi wa madini kwa wachimbaji wa dhahabu nchini,” amesema
Amesema jitihada hizo zinachukuliwa ili kutoa fursa kwa wachimbaji hao kuuza bidhaa hiyo kwa kupata punguzo la jumla ya asilimia tatu ya tozo za Serikali katika mauzo ghafi ya madini yao.
“Hatua zote hizi zinachukuliwa kwa kuzingatia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/25 katika ibara ya 65 imeielekeza Serikali kubuni na kutekeleza mipango ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kufanya kazi zao kwa tija,” amesema.
Rais Samia katika kutambua hilo alianza kuwapatia leseni wachimbaji 300 wanawake kwa kuangalia kundi la wachimbaji madini wanawake linapitia kwenye changamoto kubwa.
“Kuwatengea maeneo yenye taarifa za msingi za kijiolojia kutoa huduma za utafiti kwa gharama nafuu na kuwapa mafunzo yanayohitaji katika biashara za madini,” amesema.
Amesema Serikali jitihada zingine ni kujenga vituo na kuendesha kuwawezesha wachimbaji wadogo kujifunza teknolojia bora na yenye tija kwa uchenjuaji dhahabu.
Rais Samia ameongeza katika kutatua changamoto ya wachimbaji na wazalishaji wa chumvi mkoani Lindi, Stamico itaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha bidhaa hiyo ilikuwa na ubora unaohitajika.
“Na muwatupie jicho wazalishaji wa chumvi kwa maeneo yote ya Tanzania hasa akina mama wa mkoa wa Singida kwa muda mrefu wamejiajiri kwenye uchimbaji chumvi lakini katika eneo hilo hakuna uwekezaji uliofanyika,” amesema.