Waandishi washambuliwa kwa mikuki, mishale Ngorongoro

MASAHIHISHO: Tumelazimika kuondoa taarifa iliyokuwa hapa kuhusu tukio la waandishi wa habari kuvamiwa Ngorongoro baada ya kubaini kasoro za kimaadili, ikiwemo nia ya mwandishi, vyanzo vilivyotumika katika habari hiyo na uhakiki / ushahidi wa taarifa zilizoripotiwa.
Hata hivyo, tunatambua kuwa taarifa rasmi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) iliyotolewa usiku wa Jumanne, Agosti 15 2023 imethibitisha uwepo wa tukio hilo katika Kijiji cha Endulen kilichopo ndani ya hifadhi hiyo.
Bila kutaja idadi wala majina ya wahusika, taarifa ya NCAA imeeleza kuwa wanahabari hao pamoja na watumishi wa Serikali walivamiwa kwa kutumia silaha za jadi wakati wakitoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuhama hifadhini kwa hiyari.
Tunaomba radhi kwa yeyote aliyeathirika na ripoti yetu ya awali. Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kuhusu usahihi wa tukio hilo kwa kadiri zinavyotufikia.
Mhariri.