Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vipaumbele bajeti 2025/26

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba akiingia bungeni huku akiwaonyesha wabunge begi lililobeba hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025 / 2026, jijini Dodoma leo, Juni 12, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Gharama za Uchaguzi Mkuu, utekelezaji wa miradi ya kimkakati ni sehemu ya vipaumbele vya Serikali katika bajeti ya mwaka 2025/26.

Dar es Salaam. Kugharamia Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu na maandalizi ya viwanja kwa ajili ya michuano ya Afcon 2027, ni miongoni mwa vipaumbele vilivyowekwa na Serikali katika bajeti yake kuu ya mwaka wa fedha 2025/26.

Sambamba na vipaumbele hivyo, vingine vitakavyotekelezwa na bajeti hiyo ni utekelezaji na uendelezaji wa miradi ya kimkakati, kuimarisha sekta za uzalishaji, rasilimali watu na kuboresha mazingira ya biashara.

Hayo yameelezwa leo, Alhamisi Juni 12, 2025 na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/25, bungeni jijini Dodoma.

Katika bajeti hiyo, amesema Serikali imeweka kipaumbele cha ugharamiaji wa deni la Serikali, mishahara na stahiki za watumishi wa umma, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 na Uchaguzi Mkuu.

“Nipende kuwafahamisha Watanzania kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 tutaugharamia kwa fedha zetu za ndani,” amesema Dk Nchemba.

Maeneo mengine ya kipaumbele, amesema ni kutekeleza na kukamilisha miradi ya kimkakati, kuimarisha sekta za uzalishaji zenye matokeo chanya katika kukuza uchumi, kuimarisha rasilimali watu hususan katika sekta za huduma za jamii na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji.

Kipaumbele cha kuboresha mazingira ya biashara, kwa mujibu wa Dk Nchemba, kinalenga kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Maeneo mengine ya vipaumbele, amesema kukamilisha utekelezaji wa miradi, programu za maendeleo na afua zinazochangia maeneo makuu ya vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano.

Katika bajeti hiyo, amesema Serikali imelenga kuimarisha usimamizi wa bajeti husika kwa kuendelea kusimamia na kuimarisha matumizi sahihi ya mifumo ya Tehama katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.

“Kuimarisha uwajibikaji na udhibiti katika matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kuziba mianya ya ubadhirifu kwa lengo la kupata thamani ya fedha katika matumizi ya Serikali,” amesema.

Pia, amesema Serikali itaimarisha ufuatiliaji na tathmini katika utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha inafanywa kwa ufanisi na kuokoa gharama za ziada zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji.