Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa dini kufunzwa maadili, kudhibiti ukatili

Muktasari:

Viongozi wa dini hapa nchini wanatarajia kupewa mafunzo ya kujizuia na vitendo vya ukatili na kuwahamasisha wananchi wasijihusishe navyo

Viongozi wa dini hapa nchini wanatarajia kupewa mafunzo ya kujizuia na vitendo vya ukatili na kuwahamasisha wananchi wasijihusishe navyo

Hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa matukio ya ukatili katika jamii ambapo baadhi yanayowahusisha viongozi wa dini hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatano Oktoba 12, 2022 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Islamic Education Panel(IEP), Mohamed Kassim ambaye pia ametangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya dini kiislamu darasa la saba uliofanyika Septemba, mwaka huu amesema wana wajibu kusimamia maadili na kuzuia ukatili.

"Viongozi wa dini wanabaki kuwa wanaadamu kama walivyo wengine na wanaweza kukosa kama ilivyo kwa wengine pia wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa makosa kama ilivyo kwa wanadamu wengine isipokuwa tu ni jambo la kusikitisha kwa mtu ambaye ulimtegemea ndiye awe mwalimu wa kusimamia maadili yeye akakosa maadili hayo au akwa msimamizi mbaya wa maadili hayo.

Amesema viongozi wa dini wameona tatizo lililopo na wameliingiza katika vikao vyao mbalimbali zinavyohusisha madhehebu tofauti.

"Tunahitaji kufanya semina elekezi kwa viongozi wetu na walimu wetu juu ya dhaha hii ya maadili na mambo mengi yanayokuja sasa, kuna mambo ya ukatili, ulawiti haya yanatokea kwa hiyo tumepewa kazi ya kutoa semina elekezi kwa viongozi wetu wa dini, shuleni, madrasa na maimamu ili kulizungumzia pamoja hili kwani tunaamini kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwakumbusha kwani binadamu anatabia ya kujisahau," amesema Kassim.

Matokeo ya mitihani

Akizungumzia matokeo ya mtihani wa elimu ya dini kiislamu ya darasa la saba amesema jumla ya shule 3,710 katika mikoa 25 na halmashauri 151 zilishiriki kufanya mtihani huo ambapo waliosajiliwa walikuwa 163,143 na waliofanya mtihani ni 142,522 sawa na asilimia 87.36 huku watainiwa 20,621 wakishindwa kufanya mtihani huo kwa sababu tofauti.

"Idadi ya ya watainiwa waliofaulu kwa kupata madaraja A hadi C ni 95,166 sawa na asilimia 66.77 ya watainiwa wote. Aidha, watainiwa waliopata daraja D na E ni 47,356 sawa na asilimia 33.23 ya watainiwa wote," amesema Kassim.

Naye Amir Mkuu Baraza Kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Yussufu Kundecha amesema wanafunzi 3,567 wamefanya vizuri kwa kupata ufaulu wa alama A katika mtihani huo na ufaulu huo umeenda vizuri ikilinganishwa na mwaka jana.

"Shule 10 bora kwa kitaifa katika kundi la shule zenye watainiwa 20 au zaidi namba moja ni Mumtaaz ya Mwanza, Istiqaama ya Tabora, Rahma ya Dodoma, Algebra Islamic ya Dar es Salaam, Dumila ya Morogoro, Islamia ya Mwanza, Hedaru ya Kilimanjaro, Daarul Arqam, Mbagala Islamic na Maarifa Islamic zote za Dar es Salam." amesema Sheikh Kundecha.