Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana wengi Dar wanaishi kipato cha chini

Muktasari:

Vijana wa kiume wawili kati ya kumi wenye umri chini ya miaka 35 katika Jiji la Dar es Salaam ndio wanaomiliki kipato cha juu kinachoanzia Sh1.3 milioni kwa mwezi, sawa na asilimia mbili tu. 

Dar es Salaam. Vijana wa kiume wawili kati ya kumi wenye umri chini ya miaka 35 katika Jiji la Dar es Salaam ndio wanaomiliki kipato cha juu kinachoanzia Sh1.3 milioni kwa mwezi, sawa na asilimia mbili tu. 

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Repoa yaliyotolewa leo Septemba 28, 2022 jijini Dar es Salaam yanafafanua asilimia 85 ya kundi hilo wanaishi kwa kipato cha chini ya Sh300,000 huku wale wa kipato cha kati wakiwa asilimia 13 tu katika uwezo wa kupata Sh300,00 hadi Sh1,300,000 kwa mwezi.

Ripoti hiyo nayotokana na ukusanyaji wa takwimu kati ya Machi na Aprili, mwaka jana uliangalia ukuaji wa miji unavyoongezeka, upatikanaji wa huduma za umma kwa usawa  na michakato ya ushiriki wa wananchi katika maamuzi.