Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vifo vyafikia vinne waliofariki dunia msafara wa CCM Mbeya

Gari la serikali lililopata ajali ambalo lilikuwa limebeba waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa ziara ya Chama hicho.

Muktasari:

  • Katika ajali hiyo, watu watatu walifariki dunia papohapo, huku mwingine akifariki leo wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Mbeya. Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya barabarani ikihusisha basi kampuni ya CRN na gari la Serikali vimefikia vinne.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumanne, Februari 25, 2025 eneo la Shamwengo wilayani Mbeya ambapo basi hilo lilikuwa likilipita gari la Serikali na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo na majeruhi saba.

Waliofariki dunia papo hapo ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, Furaha Simchimba, Daniel Mselewa ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya na utingo wa basi ambaye jina lake bado halijajulikana.

Ajali hiyo ilitokea wakati msafara wa CCM, mkoani Mbeya ukitoka kumsindikiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Taifa, Fadhil Rajabu.

Leo Jumatano, Februari 26, 2025, taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala, Rodrick Mpogolo, imeeleza kufariki dunia kwa aliyekuwa dereva wa ofisi hiyo, Thadei Focus.

Focus alikuwa miongoni mwa majeruhi saba waliokuwa wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Miongoni mwa majeruhi ni waandishi Epimarcus Apolnali (Chanel Ten), Seleman Ndelage (Dream FM) na Denis George ambaye ni mwandishi wa kujitegemea.


Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi