Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu wafariki dunia msafara wa CCM Mbeya

Katibu wa Siasa na Uwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Christopher Uhagile (kulia) akizungumza wakati wa kupokea majeruhi katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Pembeni ni Spika na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson.

Muktasari:

  • Waliofariki ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, dereva wa basi la CRN na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa CCM Wilaya ya Rungwe.

Mbeya. Watu watatu wamefariki dunia akiwamo mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Mbeya, Furaha Simchimba katika ajali iliyotokea mkoani humo ikihusisha basi la Kampuni ya CRN na gari la Serikali.

Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Februari 25, 2025 katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya ambapo inadaiwa  basi lilikuwa likilipita gari la Serikali bila kuchukua tahadhari na kusababisha ajali iliyosababisha  vifo hivyo na majeruhi saba.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha kutokea  ajali hiyo akieleza kuwa kati ya majeruhi saba, wawili wapo mahututi na wengine wameruhusiwa.

"Vifo ni vitatu akiwamo mwandishi wa kujitegemea na wengine wawili ambapo tutaendelea kutoa taarifa kadri tunavyopata," amesema Kamanda Siwa.

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani hapa, Christopher Uhagile amesema ajali hiyo imetokea wakati wakitoka kumsindikiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Rajabu aliyekuwa na ziara mkoani humo.

Amesema katika ajali hiyo, wamempoteza kiongozi Daniel Mselewa ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa chama hicho, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

"Tayari CCM Taifa imeelekeza namna ya kufanya kuwasindikiza wapendwa wetu ambao ni marehemu kwa kuwa walikuwa katika majukumu ya chama,hivyo kesho tutaangalia namna ya kufanya," amesema Uhagile.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi.