Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vifo ajali ya ghorofa Kariakoo vyafika 20

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema hadi leo saa 3 asubuhi idadi ya waliofariki dunia kutokana na jengo la ghorofa kuporomoka Kariakoo jijini Dar es Salaam imefikia 20.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano Novemba 20, 2024 alipofika Kariakoo kujionea kinachoendelea, akitokea ziarani nchini Brazil.

Aidha, Rais Samia ameruhusu wafanyabiashara waliopo mbali na lilipoporomoka jengo la gorofa kuendelea na biashara zao huku walio karibu akiwataka kukaa mbali kwanza kwa muda.

Ameongeza kuwa kuendelea kushikamana kipindi hiki kama Watanzania kwasababu janga lilitokea sio la wanafamilia waliopata tu majanga bali ni la nchi kwa ujumla.

Vilevile Rais amewashukuru wananchi wote kwa mchango wao katika uokozi na msaada walioutoa Kariakoo.


Endelea kufuatilia Mwananchi.