Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Sugu aoa, wabunge 10 Chadema washuhudia

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' akimvisha pete ya ndoa mke wake, Happness Msonga katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Ruanda Jijini Mbeya. Ndoa hiyo imefungwa leo kanisani hapo. Picha na Godfrey Kahango.

Muktasari:

  • Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu leo Jumamosi Agosti 31, 2019 amefunga ndoa na Happiness Msonga katika Kanisa Katoliki Ruanda  jijini Mbeya.

Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu leo Jumamosi Agosti 31, 2019 amefunga ndoa na Happiness Msonga katika Kanisa Katoliki Ruanda  jijini Mbeya.

Katika misa hiyo wabunge 10 wa Chadema walihudhuria wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Silinde.

Wabunge hao ni  Frank Mwakajoka (Tunduma);  Anthony Komu (Moshi Vijijini); Lucia Mlowe, Sophia Mwakagenda na Lucy Mollel (wote Viti Maalum).

Wengine ni Joseph Haule (Mikumi); Joseph Selasini (Rombo); David Silinde (Momba); Pascal Haonga (Mbozi) na Wilfred Lwakatare (Bukoba  Mjini).

Viongozi wa Chadema walioshiriki misa hiyo ni mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Sadick Malila na katibu wake,  Emmanuel Masonga.