Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Meli ya Zanzibar yaungua moto

Meli mali ya kampuni ya Ocean Interprises Limited ya Zanzibar ikiwa imeteketea kwa moto agosti 14 huko katika fukwe ya bahari ya Hindi ilipokua imetia nanga kwenye bandari ya Bagamoyo kwa ajili ya kupakia mizigo mbalimbali ikiwemo Saruji na kuisafirisha Zanzibar.katika tukio hilo eneo la vyumba vya kulala mabaharia na ya kuongozea meli zimeungua kabisa na moto huo.

Muktasari:

  • Meli hiyo ilikuwa imeegeshwa kwenye fukwe iliyopo Bagamoyo, Pwani.

Bagamoyo. Meli mali ya kampuni ya Ocean Enterprises Limited ya Zanzibar imeungua moto wakati ikiwa imeegeshwa kwenye ufukwe ya Bahari ya Hindi huko Bagamoyo mkoani Pwani.

Tukio hilo limetokea leo saa 12.15 asubuhi hii wakati meli hiyo ikiwa imepaki kwenye fukwe hiyo kwa ajili ya kupakia mizigo mbalimbali ikiwemo saruji zilizokuwa zikisafirishwa  kwenda visiwani Zanzibar.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto kituo cha Bagamoyo Iward Mwanza amesema wamepokea taarifa ya moto huo saa 12.24 asubuhi na askari walifika saa 12.30 eneo la tukio.

"Ni kweli moto ulizuka kwenye hii meli na tulipata taarifa asubuhi saa 12.24 hivi tukajipanga na kufika bandarini tukakuta sehemu ya mbele ilikuwa imeshashika moto na ulikua ukiendelea kusambaa melini,”amesema.

Amesema walianza kuudhibiti ili usilete hasara zaidi na walifanikiwa.

Mkuu huyo wa zima moto Bagamoyo amebainisha kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme,

Awali kaimu ofisa mtendaji wa kata ya Dunda Sultan Mwarami amesema hadi meli hiyo inaungua haikuwa imepakia mzigo.

Amesema hakuna majeruhi wala vifo katika tukio hilo.

Kwa upande wake, nahodha wa meli hiyo Abdulrahaman Aziz amesema meli hiyo ilikuwa na watu 15, wafanyakazi 14 na nahodha wa meli hiyo.