Utalii matibabu washika kasi, huduma bora kichocheo

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo mara baada ya kuzindua magari ya kubebea wagonjwa na magari ya usimamizi shirikishi leo Oktoba 28, 2023 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Muktasari:
- Utalii wa matibabu wazidi kushika kasi idadi ya wagonjwa kutoka nje ya nchi ikiongezeka, Dar yashauriwa kujenga hosteli kwa ajili ya wagonjwa kutoka nje.
Dar es Salaam. Maono ya Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba yameanza kutimia kufuatia ongezeko la wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali ya jirani wanaoingia nchini kufuata huduma za matibabu.
Kufuatia hilo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kuangalia uwezekano wa kujenga hosteli itakayowezesha wagonjwa hao kufikia.
Ummy ameyasema hayo leo Oktiba 28, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2022/2023 hospitali za Tanzania zilipokea wagonjwa 6472 kutoka nje ya nchi.
Waziri huyo ameeleza kuwa ongezeko hilo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba na madaktari bingwa bobezi vinaivyoifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu kwa wagonjwa kutoka nchi jirani.
Waziri Ummy amebainisha kuwa Julai hadi Septemba mwaka wagonjwa waliopokelewa kutoka nje ya nchi walikuwa 1596.
Amesema wagonjwa hao walikuwa wanakuja wenyewe binafsi lakini kuanzia Novemba mwaka huu Serikali ya Zambia itaanza rasmi kuleta wagonjwa wake nchini kutibiwa saratani.
Maono yako uliyotuelekeza ya kuifanya Tanzania kuwa kinara wa tiba utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika tutafanikiwa kutokana na uwekezaji huu unaoendelea kutuwezesha.
“Jitihada zako na diplomasia yako mheshimiwa Rais umeweza kushawishi Serikali ya Zambia kuleta rasmi wagonjwa wa saratani kutibiwa katika hospitali ya Ocean Road. Tutaanza kuwapokea kuanzia Novemba.
“Niwashawishi Dar es Salaam mkuu wa mkoa muanza kujenga hosteli kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka nje ya nchi,” amesema Ummy.
Kuhusu upatikani huduma za afya waziri huyo ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka miwili Serikali imeongeza vituo 1498
“Mwaka 2021 tulikuwa na vituo vya kutoa huduma za afya 10153 leo tuna vituo 11651 ongezeko la vituo 1498 na vingi vimeanza kufanya kazi.
“Ununuzi wa mitambo na vifaa tiba vya kisasa, Tanzania hatukuwa na CT Scan katika ngazi ya hospitali za rufaa za mikoa leo mikoa yote tumepeleka mashine zote na zimeanza kufanya kazi kasoro Songwe na Mara