Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yatoa sababu kumshikilia Golugwa wa Chadema

Muktasari:

  • Golugwa amekamatwa saa 6:45 usiku Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels nchini Ubelgiji.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-bara, Aman Golugwa kwa uchunguzi wa tuhuma za kusafiri kwa siri kwenda na kurudi nje ya Tanzania.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa mchana wa leo Jumanne, Mei 13, 2025 imesema Golugwa amekamatwa saa 6:45 usiku Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels nchini Ubelgiji.

“Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa nchini.”

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuhusu suala hilo.”

Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomuhusu Golugwa.

Awali, Chadema kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X iliweka taarifa ya kukamatwa kwa Golugwa ikisema: “Alikuwa anasafiri leo Mei 13,  2025, kuelekea nchini Ubelgiji kukiwakilisha chama katika mkutano wa International Democracy Union (IDU) unaoanza kesho nchini humo.”


Endelea kutufuatilia Mwananchi na mitandao yetu.