Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uraia pacha bado, uandaaji wa hadhi maalumu uko hatua za mwisho

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo.

Muktasari:

 Suala la uraia pacha limeibuka kwa mara nyingine bungeni baada ya mbunge wa viti maalumu Suma Fyandomo kuhoji suala hilo

Dodoma. Serikali imesema kwa sasa iko kwenye hatua za mwisho za kuandaa utaratibu wa kuwapatia hadhi maalumu raia wa mataifa mengine wenye asili ya Tanzania ili kuchangia maendeleo ya nchi yao ya asili.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo jana Aprili 5, 2024 wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Suma Fyandomo (CCM).

Mbunge huyo amehoji kwa nini Tanzania hairuhusu uraia pacha.

Akijibu swali hilo, Sillo amesema uraia wa Tanzania unasimamiwa na Sheria ya Uraia ya Tanzania Sura ya 357 rejeo la mwaka 2002.

Sheria hii inabainisha aina tatu za uraia wa Tanzania ambazo ni uraia wa kuzaliwa, uraia wa kurithi na uraia wa kujiandikisha.

Amesema kwa mujibu wa sheria hiyo, Serikali hairuhusu uraia pacha kwa watu wazima isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18.

Katika swali la nyongeza, Fyandomo amehoji kuna ugumu gani serikali kuruhusu uraia pacha kama ilivyo nchi nyingine ambazo zinanufaika na raia walio nchi za nje.

Amesema nchi jirani ya Kenya kupitia uraia pacha inaingiza fedha za kigeni Dola 4.2 bilioni za Marekani na Tanzania kupitia mambo ya uraia inaingiza Dola 520 milioni  za Marekani.

Mbunge huyo amehoji Serikali haioni kuruhusu uraia pacha kutaongeza mapato ya nchi.

Akijibu swali hilo, Sillo amesema mchakato wa kutoa hadhi hiyo itakapokamilika wananchi hao watachangia maendeleo ya nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema kutokuwa na uraia pacha sio sababu ya Watanzania kutochangia maendeleo.

"Serikali imeshaamua kuwa kutoa hadhi maalumu na miamala kutoka nje ya nchi imekuwa ikiongezeka, hata hivyo hapo baadaye Serikali itakapoona kama kuna umuhimu wa kutoa uraia pacha mchakato wake utafanyika," amesema.