Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diaspora wapinga msimamo wa Tanzania kuhusu uraia pacha

Mwakilishi wa kundi la Watanzania waishio nje ya nchi, Liberatus Mwang’ombe.

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema iko katika mchakato wa kutoa Hadhi Maalum kwa wananchi wake wanaoishi nje ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Imesema uraia pacha kwa sasa haiwezekani kwani halina muafaka nchini na nje ya nchi.

Dar es Salaam. Mwakilishi wa kundi la Watanzania waishio nje ya nchi, Liberatus Mwang’ombe amesema msimamo wa Serikali kuhusu pingamizi la uraia pacha halitakuwa na manufaa kwa Taifa.

 Ametoa angalizo la kukubaliana na hadhi maalumu inayotolewa kama mbadala.

“Hadhi maalumu ni risiti ya kuukana uraia wa Tanzania, hata ukienda mahakamani itabidi watumie kielelezo hicho, yeyote atakayechukua hadhi maalumu atakuwa amechukua risiti ya kuukana uraia pacha. Serikali imesema,” amesema Mwang’ombe.

Mwang’ombe anayeishi nchini Marekani ametoa kauli hiyo leo Mei 31, 2023 wakati akichangia mada kwenye Twitter Space ya Mwananchi Communications Limited (MCL) yenye mada ‘una maoni gani kuhusu suala la uraia pacha Tanzania.’

Amesema zaidi ya Diaspora 1,000 hawakubaliani na msimamo huo wa Serikali, akisema asilimia 74 ya mataifa duniani yanakubaliana na uraia pacha.

Aidha, amesema hadhi maalumu ni tishio pia linaloweka mtegoni Watanzania waishio nje katika uwekezaji wa mali zao. Amesema hadhi hiyo inaweza kufutwa wakati wowote kutokana na matakwa wa kiongozi aliyeingia madarakani kwa wakati husika.

“Anaweza kuingia kiongozi mpya madarakani na kuifuta hadhi hiyo kwa hiyo unaweza kuwekeza mali na ikafutwa na ukapoteza mali zote,” amesema.

Anachokisema Mwang’ombe kinaungwa mkono na Abiud Paranjo, Mtanzania anayeishi nchini Marekani ambaye ameshauri Serikali kutengua msimamo wake kuhusu uraia pacha, akisema kuzaliwa Tanzania haikuwa chaguo lake.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax akiwasilisha bajeti ya wizara yake Jumanne ya Mei 30, 2023 alilieleza Bunge kuwa Serikali,“ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuwapatia Hadhi Maalum Diaspora wenye asili ya Tanzania na uraia wa nchi nyingine.”

Waziri Tax alisema wizara ilikusanya maoni toka kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Diaspora.


Alisema maoni yameainisha maeneo/masuala yanayopendekezwa kujumuishwa katika Hadhi Maalum.

Waziri Tax alisema bado suala la uraia pacha halina muafaka nchini na nje ya nchi.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuhakikisha diaspora ambao wako nchi za nje ni raia wenye asili wote wanapata haki na kutoa msisitizo wafanye mchakato wa kutoa hadhi maalum.

“Ukitoa uraia pacha kwa sasa hivi wakati hakujawa na muafaka kitaifa na kidunia kuna wale wanaoweza kukosa fursa. Kuna nchi ambazo diaspora zipo na zile hazitambui uraia pacha. Sisi tukitoa uraia pacha wale hawatapata fursa ambazo tunatarajia kuzitoa,” alisema.