Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upelelezi kesi ya Mkurugenzi Jatu wakamilika

Muktasari:

  • Upande wa mashtaka wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa upelelele wa kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh5.1 bilioni, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (32) umekamilika.

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa upelelele wa kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh5.1 bilioni, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (32) umekamilika.

 Wakili wa Serikali, Jaribu Bahati ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatatu Machi 13, 2023, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa hakimu, kesi hii imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake umekamilika hivyo tunaomba terehe nyingine kwa ajili ya kumsomea hoja za awali (PH) mshtakiwa huyu," amesema wakili Bahati.

Hakimu Mrio amekubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 27, 2023 itakapoitwa kwa ajili upande wa mashtaka kumsomea hoja za awali mshtakiwa huyo.

Hata hivyo, leo mshtakiwa huyo hakuletwa mahakamani isipokuwa kesi hiyo ilisikilizwa kwa njia ya video huku mshtakiwa akiwa mahabusu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Gasaya andaiwa kutenda kosa hilo katika ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika Jiji la Dar es Salaam, akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia Sh 5,139,865,733 kutoka Saccos ya JATU.

Mshtakiwa anadaiwa kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka Saccos ya JATU kwa kujipambanua kwamba fedha hiyo ataipanda kama sehemu ya uwekezaji ili kuzalisha faida zaidi jambo ambalo alijua kuwa sio kweli.