Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umeme wakwamisha mahakama kutoa uamuzi dhamana Mkurugenzi wa Jatu

Muktasari:

  • Mshtakiwa huyo anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya Jatu kwa madai kuwa fedha hizo anazipanda ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kutoa uamuzi katika kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh5.1 bilioni, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jatu  PLC, Peter Gasaya, baada ya umeme kukatika katika Gereza la Keko.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya Jatu kwa madai kuwa fedha hizo anazipanda ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Kesi hiyo iliitwa leo Jumatatu Februari 27, 2023 kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo mahakama hiyo inampunguzia masharti ya dhamana mshtakiwa huyo ili aweze kupata dhamana au inayatupilia mbali maombi yake aliyowasilisha mahakamani hapo akiomba apunguziwe masharti.

Hata hivyo kesi hiyo iliyokuwa inasikilizwa kwa njia ya Video Comference ilishindwa kuendelea baada ya umeme kukatika sehemu ambayo imetengwa maalumu kwa ajili ya kusikilizia kesi kwa watuhumiwa waliopo katika mahabusu Gereza la Keko.

Kutokana na umeme kukatika katika gereza hilo wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa,  Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio anayesikiliza shauri hilo, aliahirisha kesi hiyo hadi kesho, Februari 28, 2023 atakapotoa uamuzi dhidi ya mshtakiwa huyo.

Itakumbukwa kuwa Januari 2, 2023, mahakama hiyo ilitoa masharti ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo kwa kumtaka kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslimu Sh 2.6 bilioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia ilimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha fedha taslimu Sh 2.6 bilioni au isiyohamishika yenye thamani hivyo.

Haya hivyo mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana siku hiyo na badala yake aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba impunguzie masharti ya dhamana ili ajidhamini.

Kupitia wakili wa mshtakiwa huyo, Nafikire Mwamboma, aliomba mteja wake  mahakama impunguzie masharti ya dhamana kutoka Sh 2.6bilioni alizotakiwa kuwasilisha mahakamani hapo hadi Sh200 milioni au Sh150 milioni.

Mbali na ombi hilo, Gasaya aliomba mahakama hiyo kupitia upya masharti ya dhamana ya dhidi yake, kwa sababu masharti aliyopewa ni magumu na ndio maana ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Gusaya baada ya kuwasilisha maombi yake, Serikali ilijibu hoja zake kwa kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya mshtakiwa ya kupunguziwa masharti ya dhamana na mahakama kwa maelezo kuwa masharti yaliyotolewa na mahakama hiyo ni ya haki kulingana na sheria iliyopo isipokuwa Gasaya mwenyewe ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Awali, wakili wa Serikali, Caroline Matemu alidai mahakmani hapo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya uamuzi na upande wa mashtaka wapo tayari kusikiliza.

Katika kesi ya msingi, Gasaya andaiwa kutenda kosa hilo, katika ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika jiji la Dar es Salaam, akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia Sh 5,139,865,733 kutoka Saccos ya JATU.

Mshtakiwa anadaiwa kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka Saccos ya Jatu kwa kujipambanua kwamba fedha hiyo ataipanda kama sehemu ya uwekezaji ili kuzalisha faida zaidi jambo ambalo alijua kuwa siyo kweli.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo Desemba 29, 2023 kujibu shtaka linalomkabili.