Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulinzi waendelea kuimarishwa kanisani kwa Askofu Gwajima, waumini wasali barabarani

Muktasari:

  • Makundi ya waumini wa kanisa hilo wamesimama maeneo mbalimbali ya Kanisa hilo wakiwa wanatazama kile kinachoendelea.

Dar es Salaam. Ulinzi umeimarishwa kwenye viunga vya Kanisa Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Juni 2, 2025, Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo kutokana na kukiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kile alichoeleza limekuwa linatoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa.

Tangu wakati huo, kanisa hilo limekuwa likilindwa na askari Polisi wenye silaha. Hata hivyo, kadri siku zilivyokwenda, ulinzi ulipungua huku utepe uliowekwa kuzuia watu kuingia na kutoka uliendelea kusalia.

Kanisa hilo, limefungua kesi mahakamani kupinga hatua hiyo na kesi inaendelea.

Jana Jumamosi, Juni 14, 2025 kupitia mtandao wa kijamii wa Askofu Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (CCM) jijini Dar es Salaam, alitangaza uwepo wa kusanyiko akiandika: “Waebrania 10:25, wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.”

Asubuhi ya leo Jumapili, Juni 1, 2025 Mwananchi limefika eneo la kanisa hilo na kukuta askari wakiwa wametanda maeneo mbalimbali kuhakikisha hakuna anayeingia kanisani hapo.

Katika eneo hilo, askari polisi wamesimama kulizunguka kanisa hilo upande wa mbele huku kukiwa na utepe wa njano ikiashiria ni eneo lililodhibitiwa.

Askari wengine wanatembea na magari ya polisi maarufu kama 'difenda' upande wa pili wa barabara hiyo ya Morogoro.

Baada ya waumini kukaa makundi makundi nje ya kanisa huku askari wakiwafuata kuwatawanya kwa kuwaambia hatimaye wamekusanyika kufanya maombi kwa pamoja.

Waumini hao wamekusanyika saa 4:45 asubuhi hii wakifanya maombi pembeni ya barabara ikiwa ni mita chache kutoka kanisani hapo.

Sababu ya kufanya hivyo ni baada ya askari kuweka uzio wa utepe kutoingia kanisani baada ya kanisa hilo kufutwa.

Wakati wameanza maombi gari la askari lilikuwa limesimama huku askari wakiwatazama wakiendelea na maombi.

Baada ya dakika kadhaa askari hao waliondoka na gari wakielekea usawa wa kanisa hilo.

Waumini hao wameonekana kusali kwa mtindo wa kutembea licha ya magari na pikipiki kupitia katika eneo hilo.

Endelea kufuatilia Mwananchi