Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TSC yabaini madai kwa walimu 136,000, Mchengerwa aagiza yamalizwe haraka

Muktasari:

Baada ya Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC) kubaini walimu wenye changamoto za stahiki zao, Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo kwa maofisa utumishi wa halmshauri.

Dodoma. Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC) imebaini walimu 136,000 wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za stahiki zao.

 Kufuatia hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa ameagiza maofisa utumishi nchini kutumia siku 14 kuhakikisha hakuna mwalimu anayeachwa.

Mchengerwa amesema hayo leo Jumamosi, Februari 3, 2024 wakati akifungua kikao kazi kinachotoa fursa ya kushughulikia changamoto ya upandishwaji vyeo na kubadilishwa kada kwa walimu.

Katika ufunguzi huo, waziri huyo amekabidhi magari 13 ya kusaidia uendeshaji na ufuatiliaji wa elimu ya awali na msingi katika halmashauri 13 kupitia mradi wa GPE-Lanes yenye gharama ya Sh bilioni 1.8.

Pia, shughuli hiyo imeambatana na ugawaji wa vifaa vya Tehama kwa ajili ya shule za msingi 200 kupitia mradi wa BOOST.

Akizungumza, Mchengerwa amesema ameiagiza tume hiyo kufanya uchambuzi ili kubaini walimu wote wenye changamoto katika upandaji wa vyeo na walimu zaidi ya 136,000 wamebainika kuwa na changamoto mbalimbali.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha malalamiko yote ya walimu yanashughulikiwa na ameagiza uhakiki wa kina ufanyike na uhusishe taarifa za utumishi zilizo kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara.

Mchengerwa amesema kwa kufanya hivyo kumewasaidia kupata taarifa zote za walimu walioko katika maeneo mbalimbali.

“Rais anataka kila mmoja wetu katika wizara hii ya Tamisemi kufuatilia kwa msingi, haki za kila mwalimu, kupekuwa, kutafuta na kusahaulika kwa changamoto za walimu mara moja. Niwapongeze kwa kuanza kazi hii mara moja,” amesema.

Amewapongeza wa hatua ya kupata malalamiko ya walimu 136,000 lakini akasema dhamira ya Rais ni kutotaka aachwe mwalimu mmoja hata mmoja katika kushughulikiwa changamoto alizonazo.

Amesema kazi hiyo itafanyika kwa takribani siku 14 na kuagiza kuifanya bila upendeleo kwa kuangalia haki ya kila mmoja, ili waweze kuwajenga katika imani na moyo wa kuendelea kutoa elimu katika maeneo yao.

“Ili waendelee kutoa elimu kwa watoto wetu, elimu hiyo iwe itakayokwenda kuwafaa watoto wetu kwa maisha ya kesho. Imani yangu baada ya kazi hii kukamilika changamoto za walimu zitakwenda kushughuhulikiwa kikamilifu,” amesema.

Aidha, Mchengerwa ameagiza maofisa hao kushughulikia haki za walimu hata wanaoumwa (wako kitandani) na wale wenye dharura za ugonjwa, ili kurekebisha kasoro zilizokuwepo kama Rais Samia Suluhu Hassan anavyosisitiza wakati wote.

Aidha, Mchengerwa ameagiza wakurugenzi ambao hawajawalipa maofisa utumishi waliokwenda kuhakiki changamoto za walimu wawe wamewalipwa hadi kufikia Jumatatu (kesho kutwa).

“Katibu Mkuu ikifika hadi saa 12 jioni Jumatatu niletee orodha ya wakurugenzi ambao hawajawalipa stahiki za maofisa utumishi, ili nichukue hatua mara moja. Ninatarajia mtakuwa makini na kufanya kazi hii kwa ufanisi, ili kuhakikisha hakuna mwalimu atakayeachwa baada ya zoezi hili kufanyika.

 “Naomba niweke wazi, sitamvumilia mtendaji yeyote ambaye hatawajibika kushughulikia kero za walimu na sitamani kusikia walimu wana malalamiko kuhusu masilahi yao ya kiutumishi,” amesema.

Aidha, Mchengerwa ameagiza hadi kufikia Jumatatu ya Februari 5, 2024 saa 12 jioni wakurugenzi wahakikishe wanawalipa posho maofisa 62 wanaoshiriki kikao hicho.

Awali, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia elimu, Dk Charles Msonde amesema pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na TSC wameamua kufanya kikao kazi cha siku 14 cha maofisa utumishi wa halmashauri nchini, lengo ni kuhakiki taarifa za walimu.

“Kutokana na maelekezo yako ya kuhakikisha malalamiko ya walimu yanashughulikiwa kwa ufanisi na hakuna anayeachwa, tumeamua kufanya kikao kazi cha siku 14 cha maofisa utumishi wa halmashauri ili kuhakiki taarifa za walimu,”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tamisemi, Denis Londo amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema uandikishwaji wa wanafunzi katika Mkoa wa Dodoma mpaka juzi Alhamisi umefikia asilimia 92 kwa upande wa elimu ya awali, asilimia 95 na kwa darasa la kwanza na asilimia 67.

Pia ameahidi kwa niaba ya wakuu wa mikoa wengine kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa magari na vifaa vya Tehama ambavyo vimeelekezwa katika maeneo yao.