Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu tatu kuchunguza ajali ya ndege ya Precision

Ndege ya Precision Air iliyopata ajali Ziwa Victoria Novemba 6, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 24 ikitolewa kwenye maji.

Muktasari:

  • Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amezitaja timu tatu zitakazochunguza ajali ya kampuni ya Precision iliyotokea Novemba 6 Bukoba, mkoani Kagera, kuwa ni pamoja na Kitengo maalum cha uchunguzi cha ajali za anga, kampuni iliyotengeneza ndege na Kampuni iliyotengeneza injini.

Bukoba. Serikali imesema timu tatu zinatarajia kufanya uchunguzi ajali ya ndege ya Precision Air yenye namba za usajiri ATR 42-5H PWF iliyotokea Bukoba mkoani Kagera.

Hayo yamesemwa leo Novemba 08, 2022 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Amesema kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 06, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 26 tayari timu za uchunguzi zimeanza uchunguzi.

Ametaja timu zinazohusika kuwa ni pamoja na Kitengo maalum cha uchunguzi cha ajali za anga ambacho kilishaanza kufanya kazi za awali, kampuni iliyotengeneza ndege na Kampuni iliyotengeneza injini.

Msigwa amesema miili 19 ya marehemu 16 imeishasafirishwa na ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya mazishi bado miili mitatu miwili itasafirishwa kwenda nchini Kenya na mmoja wa Uingereza wanafanya taratibu za mawasiliano.

Kuhusu kijana Majaliwa Jackson amesema, taratibu za kumsajiri katika jeshi la zimamoto na uokoaji zinafanywa na jeshi hilo na atapelekwa Tanga kwa miezi 4 kwa ajili ya mafunzo.