Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miili ya wawili waliofariki ajali ya ndege yawasili Arusha

Mwili Aneth Kaaya ukipokewa katika Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru

Muktasari:

Ajari hiyo ya ndege ilihusisha ndege aina ya ATR 42-500 ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba na ilipotaka kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba iliangukia ziwani, mita 100 kutoka ulipo uwanja wa ndege.

Arusha. Miili ya abiria wawili kati ya 19 waliofariki kwenye ajali ya ndege Precision Air iliyotakea Novemba 6, 2022 mkoani kagera imewasili mkoani Arusha kwa ajili ya maziko.

Miili hiyo ni ya Aneth Kaaya na Zaituni Mohamed  ambao wamepokewa na Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na familia zao katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na hospitali ya Seliani na wanatarajiwa kuzikwa kesho.

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru baada ya kupokea miili hiyo, Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema mwili wa Zaituni umehifadhiwa katika hospitali ya Seliani huku wa Aneth ukihifadhiwa Mount Meru.

"Tunaendelea kushukuru Mungu miili hiyo imefika salama ikiongozwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kagera," amesema.

Naye Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Christopher Pallangyo amesema wamesafirisha miili mitatu ikiwa mmoja umeachwa wilaya Kondoa mkoani Dodoma kwa ajili ya mazishi.

"Miili miwili ni hii ambayo ni ya wadada zetu hivyo tunashukuru Mwenyezi Mungu tumesafiri salama kwani hatujapata tatizo lolote tukiwa njiani,"amesema Pallangyo.

 Kaka wa marehemu Aneth, Frank Lameck amesema anaishukuru Serikali kwa kufanikisha mwili wa ndugu yao kufika nyumbani kwani alikuwa njiani kuelekea ukweni kutambulishwa lakini hakufanikiwa kutokana na umauti kumfika.

Lameck amesema Aneth ambaye alifariki akiwa anaenda kutambulishwa ukweni alikuwa anajishughulisha na biashara ya uuzaji wa duka la vipodozi Dar es Salaam.

"Kitu alichokuwa anakifuata Bukoba hakijafikia lengo lake lakini hayo yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na ikiwa tu tumewasiliana kwa njia ya jumbe wasapu tukitaniana tu kwa wiki mbili zilizopita kweli alikuwa ni mtu wa watu sana,"amesema Lameck.