Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tetemeko la ardhi lapiga Japan, tahadhari ya tsunami yatolewa

Muktasari:

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.3 katika kipimo cha Richter limepiga nchini Japan huku tahadhari ya kutokea kwa tsunami ikitolewa.

Japan. Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.3 katika kipimo cha Richter limepiga nchini Japan huku tahadhari ya kutokea kwa tsunami ikitolewa.

Tetemeko hilo limetokea leo Jumatano Machi 16, 2022 na kusababisha kukatika umeme kwenye kaya zaidi ya milioni 2 na uharibifu wa vitu mbalimbali. 

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imesema kuwa polisi wanafanya tathmini kujua kiwango cha uharibifu kilichosababishwa na tetemeko hilo.

Muda mfupi baada ya tetemeko hilo mamlaka nchini humo zilitoa tahadhari ya mawimbi ya tsunami katika Pwani za Fukushima na Miyagi.

Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha uharibifu wa vitu yakiwamo majengo.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amewaambia waandishi wa habari kuwa Serikali inakusanya taarifa za madhara yaliyotokana na tetemeko hilo.

"Tutajitolea kukusanya taarifa, kufanya kila tuwezalo kuwaokoa walioathirika na tetemeko na kuwasilisha taarifa ipasavyo," amesema.