Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tarura yapongezwa mradi wa barabara Nyasa

Nyasa. Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Abdallah Kaimu amepongeza viongozi wa Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) wilaya ya Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma  kwa kutekeleza  mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami nyepesi kwa weredi na uaminifu .
Pongezi hizo amezitoa jana wakati akiweka jiwe la msingi katika  mradi wa ujenzi wa barabara yya Mbamba Bay kuelekea kituo cha afya kilichopo wilayani Nyasa ambao umetekelezwa na mkandarasi M/S Luke kwa ufadhili wa fedha za mfuko wa majimbo.

Akizungumza na wananchi Kaimu amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo baada ya kukagua nyaraka na kujiridhisha kuwa hazina tatizo, pia barabara imejengea kwa viwango na ubora unaotakiwa .

 Amesema ameridhishwa na utendaji wa kazi wa Tarura kwani  wameonyesha jitihada na nidhamu katika utekelezaji wa miradi ya barabara mkoani humo .

"Nimetembelea na kukagua mradi wa barabara kiwango cha lami nyepesi wilaya ya Nyasa, nimekagua nyaraka na kujiridhisha  hivyo mwenge wa uhuru umeridhia kuweka jiwe la msingi katika mradi huu," amesema Kaimu

Awali akitoa taarifa kwa kiongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa , Meneja Tarura Nyasa, Mhandisi Thomas Kitus alisema mradi huo umegharimu Sh500 milioni fedha ambazo ni za serikali kuu.

Alisema mradi huo umetekelezwa kwa siku 120 kuanzia Oktoba 28, 2022 hadi Februari 27, 2023 ambapo hadi sasa mradi umekamilika kwa asilimia 99 na bado upo kwenye matazamio.