Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tarura yapiga marufuku kupitisha ng’ombe barabarani

Siha. Wananchi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wameonywa kuacha kupitisha mifugo katika barabara zilizojengwa kwa kiwango cha changarawe kwenye maeneo yao ili ziwezi kudumu kwa muda mrefu.

Pia kuacha kuharibu mifereji ya kupitisha maji iliyopo pembezeni mwa barabara hizo na kusababisha maji kukosa muelekeo na kusambaa juu ya barabara

Meneja wa Wakala wa Barabara za mijini na Vijiji (Tarura) wilayani humo, Protias Kawishe akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya wilaya kutembea ujenzi wa miradi ya nyanja mbalimbali ya barabara, ametaka wananchi kulinda barabara hizo ili ziweze kukaa kwa muda mrefu.

"Ni kweli Watu wanapitisha mifugo hasa ukanda wa tambarare na hawa wa ukanda wa juu wao wanapitisha mifereji ya umwagiliaji juu ya barabara baada ya miezi miwili au mitatu  zinakuwa hazipitiki tena zinakuwa zimeharibika,"amesema Kaweshi.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya ukarabati barabara ambazo zimejengwa kwa muda mfupi kutokana na tatizo hilo.

Hivyo amewaomba wananchi kulinda miundombinu mbinu hiyo ili iweze kukaa kwa muda mrefu na kuokoa fedha za Serikali kutengeneza barabara hizo mara kwa mara.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Wilfred Mosi amesema kuhusu kulinda barabara hizo wameongea na meneja huyo wa Tarura kuitisha mikutano ya kijiji ili waweze kuelimisha juu ya utunzaji wa barabara.

Amesema barabara hizo zinajengwa kwa fedha nyingi kwa hiyo ni muhimu kutunzwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kupitika kwa wakati wote, tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha nyingi kwenye miradi katika wilaya yetu.

Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka, ametaka Wananchi kushirikishwa kwenye miradi inayojengwa kwenye maeneo yao.

Amesema miradi kama itafanywa bila ya wao kushirikishwa, hawaoni kama ni mali yao, kwa hiyo wao wakishirikishwa watakuwa na uchungu na huo mradi.