Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kutokomeza Ukimwi ifikapo 2030, yaita wadau

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Wilson Charles akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa mbio za ATF Marathon zilizofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro huku Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk Jerome Kamwela akishuhudia.

Muktasari:

  • Tanzania imeweka mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo 2030, mkakati huo unawiana na ule wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi (UNAIDS).

Dar es Salaam. Serikali imewaomba wadau kuunga mkono juhudi na mikakati yake ya kukabiliana kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na imetangaza kuwa iko kwenye utekelezaji wa kuutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.

Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Wilson Charles wakati wa Mbio za Nyika (ATF Marathon), zilizofanyika viwanja vya shule ya Sekondari ya Morogoro ambazo zilitumika kama sehemu ya kuchochea maadalizi ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika kitafa mkoani humo, Desemba Mosi.

Wakati Tanzania ikiweka mikakati hiyo ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030, Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi (UNAIDS), limeonyesha matumaini ya kutokomeza ugonjwa huo 2030.

Kwa mujibu wa ripoti yake ya kila mwaka ya siku ya Ukimwi duniani, UNAIDS limetangaza kuwa kuna watu milioni 39 wanaoishi na virusi vya Ukimwi duniani kote.

Kwa upande mwingine, takwimu kutoka Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa hadi Machi 2023, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 1.7 wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Kati yao, imeelezwa kuwa watu 1.6 sawa na asilimia 94.4 ya wanaoishi na ugonjwa huo wanatambua hali zao za maambukizi na kati yao, asilimia 98.8 wako kwenye dawa za kufubaza VVU (ARVs).

Pia asilimia 96.6 ya wanaotumia ARVs, wamefikia kiwango cha chini cha VVU mwilini.

Dk Charles amewataka wadau na wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutokomeza maambukizi hayo, huku kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ikitoa Sh17 milioni kama sehemu ya mchango wake.

"...napongeza juhudi zinazochukuliwa na wadau wetu ikiwamo GGML pamoja wananchi...michago hii inazolenga kutunisha Mfuko wa Udhibiti wa Ukimwi (ATF) na kuunga mkono sera ya 'Tokomeza Ukimwi, Tanzania bila Ukimwi inawezekana," amesema Dk Charles na kuongeza:

"Nipende kuwapongeza wote kuunga mkono...na mna nia ya kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha malengo ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2030 yanafanikiwa."

Akizungumzia ushiriki wa GGML, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Stephen Mhando amesema mchango huo ni moja ya jitihada za kampuni hiyo katika kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi juu ya ugonjwa huo na kuutokomeza ifikapo 2030.

"Ufadhili huu wa GGML unathibitisha dhamira ya dhati ya kampuni yetu kudumisha uendelevu kwa watu wote. Kwamba tunalenga kuhakikisha kuwa jamii inayozunguka shughuli za mgodi wetu na hata walio nje ya Geita wanafaidika na uwepo wa kampuni hii.

"Fedha hizi tunaamini zitagusa moja kwa moja maisha ya watu wanaoishi na VVU... Geita ikiwa moja ya mikoa yenye idadi kubwa ya wachimbaji madini ikiwamo walio na wasio na VVU, kwetu sisi ni vigumu kukwepa jukumu kama hilo la kuwajali watu wa aina hii na kuwawezesha kwa namna mbalimbali." amesema

Kwa upande wake, Mshiriki wa ATF Marathon, Neema Matheo amesema mazoezi ni muhimu kwa mwili wa mwanadamu kwani bila mazoezi mwili huweza kupata magonjwa  yasiyoambukiza kwa haraka na urahisi zaidi yakiwemo ugonjwa wa Moyo na Kisukari.

Katika mbio hizo mshindi wa kwanza wa kilomita 21 alipata zawadi ya Sh300,000, mshindi wa pili Sh250,000 na wa tatu Sh200,000 vivyo hivyo kwa upande wa washindi wa mbio za baiskeli kilomita 66.

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, mwaka huu kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro, yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Jamii iongoze kutokomeza Ukimwi". Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mwisho.