Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya wahamasishwa kutumia ATM maalumu kupima VVU

Mwelimisha rika wa VVU katika ngazi ya jamii kutoka shirika la HJFMRI Sasha Mohamed (kulia) akitoa maelezo kwa  Mkurugenzi mkazi wa WRAIR Mark Breda baada ya kutoa kipimo cha VVU cha Jipime pamoja na kondomu za bure kwenye "ATM" maalum inayotoa huduma hizo  Jijini Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Mashine za ATM zilizozinduliwa leo Jijini Mbeya zitafungwa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kumbi za starehe, vyuo vikuu kwa lengo la kuwasaidia wananchi kujipima na kukijinga na maambukizi mapya ya VVU.

Mbeya. Wananchi mkoani hapa wamehamasishwa kutumia mashine maalumu za kisasa (ATM) zinazotoa huduma za bure za kipimo cha Virusi Vya Ukimwi (VVU), maarufu kwa jina la ‘Jipime’ ili kutambua afya na kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.

Hayo yameelezwa leo Novemba 21, 2023 na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Mark Breda alipokuwa akizindua ATM maalumu ya kutolea vipimo hivyo jijini hapa.

Breda amesema uwepo wa mashine hizo utakuwa fursa kwa vijana kuendelea kuchukua tahadhari, ili kuepuka maambukizi mapya ya Ukimwi kwa kulinda afya zao na kujenga uelewa mzuri wa uzalishaji mali.

“Serikali ya Marekani kupitia WRAIR tumefanikiwa kufadhili upatikanaji wa mashine hizi zitakazosambazwa Mkoa wa Mbeya na mikoa yote ya nyanda za juu Kusini kupitia Shirika la HJF Medical Research International (HJFMRI), ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za VVU katika jamii,” amesema Mark.

Ka upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la HJFMRI linalosambaza vipimo hivyo, Sally Chalamila amesema lengo ni kuwafikishia wananchi huduma katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vipimo vya jipime na mipira ya kiume (kondom).

“Vipimo hivyo vitapatikana bure na kila mwananchi ataweza kujipima kupitia maelezo yaliyopo kwenye mashine, endapo kitaonyesha kuwa na maambukizi anatakiwa kufika kwenye kituo cha afya ili kufanya kipimo cha uhakikisho,” amesema.

Sally amesema mikakati ya shirika hilo ni kuwezesha   kutoa huduma za dawa kinga maarufu kama PrEP hususani kwa Mkoa wa Mbeya.

Amesema ATM hizo  zitafungwa kwenye kwenye maeneo yote ya starehe, vyuo vikuu na yenye mikusanyiko ya watu.

“Katika utekelezaji wa afua za Ukimwi tumegundua  changamoto ya maambukizi mapya ya VVU yapo kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 24, ambapo hali ya maambukizi mapya ikiwa ni asilimia 40, huku vijana wa kike wakiwa asilimia 80 na wa kiume ikiwa ni asilimia 20,”amesema.

Amesema shirika hilo linatekelezaji afua za matunzo na matibabu ya Ukimwi kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Wizara ya Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi) kupitia usimamizi wa afya ngazi za  halmashauri hususani mikoa ya Mbeya, Songwe Rukwa na Katavi, huku mkoani Ruvuma likitekeleza afua ya tohara ya hiari kwa wanaume.

Akizungumza na Mwananchi, mfanyabiashara wa mitumba nje ya Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya, Peter Thobias amesema mfumo huo wa mashine utasaidia kupunguza udanganyifu na vijana kuwa na hofu ya kufanya ngono zisizo salama.