Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanesco yaweka rekodi faida yake ikifikia Sh109 bilioni

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande akizungumza katika moja ya tukio ya shirika hilo. Picha na Mtandao

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limevuna faida ya Sh109 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/2022.
 Hayo yalielezwa jana na Mkurugezi Mtendaji wa shirika hilo, Maharage Chande alipozungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
 Alisema Tanesco kwa mara ya kwanza ilijiwekea rekodi hiyo mpya kwa sababu walifanikiwa kuzungumza na mwanahisa wao (Serikali) ambayo ilibadilisha deni ililokuwa ikidaiwa kuwa mtaji.
Itakumbukwa Tanesco ilikuwa inadaiwa Sh950 bilioni na kampuni za IPTL, Songas, Pan African na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), huku Sh442 bilioni ilizikopa benki kwa matumizi mbalimbali.
Katika mkutano huo uliolenga kueleza kazi na mafanikio ya Tanesco, Chande alisema faida hiyo inalifanya shirika hilo kuwa vizuri kwenye vitabu vya faida na hasara.
Mbali na faida hiyo, Chande alisema mapato ya Sh1.8 trilioni waliyoyapata mwaka 2021/2022 haijapata kutokea ndani ya Tanesco.
Kwenye mtiririko wa fedha, alisema Tanesco limefanya vizuri lakini hawajafikia lengo.
“Mwaka jana tulikuwa hasi ya Sh200 bilioni, mwaka huu tupo hasi Sh125 bilioni na hii ndio mipango yetu ndani ya miezi 24. Tunataka safari hii tupate chanya Sh50 bilioni,” alisema.
Ili kufikia hatua hiyo, Mkurugenzi wa Fedha, Renata Ndege alisema wamewekeza nguvu katika matumizi ya teknolojia, kufanya manunuzi ya kimkakati, kutumia watoa huduma wengine na kutoa huduma kwa njia ya mtandao.
Alitaja mikakati mingine ni kujikita katika matumizi ya mita za kisasa (Smart Meter), kukamilisha mradi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na kuboresha kitengo cha kuhakiki mapato.
Kwa upande wake, Makamu mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya akizungumzia uzalishaji wa umeme, alisema asilimia 33 ya umeme unaoingia kwenye gridi ya Taifa unatokana na maji na asilimia 67 unachangiwa na gesi asilia.
Kutokana na hayo, gharama za uzalishaji umeme zimeongezeka kutoka Sh1.6 trilioni mwaka 2020/2021 kufikia Sh1.8 trilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.
Kuhusu upotevu wa umeme, Pakaya alisema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa asilimia tisa, lakini kufikia 2021/2022 ulipungua na kufikia asilimia nane.
“Upotevu wa umeme ukipungua maana yake umeme unaenda kwa mteja moja kwa moja, ndiyo maana mapato yameongezeko,” alisema.
Kinachochangia upotevu wa umeme alisema ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotevu huo.


Gharama za umeme
Awali, Chande alisema kukamilika kwa bwawa la Julius Nyerere Juni 2024, hakutapunguza bei ya umeme, bali kutapunguza gharama za uendeshaji.
“Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za uendeshaji zitashuka, lakini hatutashusha bei kwa sababu tutashindwa kwenda," alisema.
Idadi ya wateja ambao wangenufaika na punguzo la bei ya umeme ni milioni 4.4, ambao mpaka sasa shirika hilo linawatambua, miongoni mwao 4,000 ni wateja kutoka viwandani na waliobaki ni watumiaji wa nishati hiyo nyumbani.