Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanesco yataja sababu mikoa kadhaa kukosa umeme

Muktasari:

  • Mikoa kadhaa nchini imekumbana na changamoto ya kukosa umeme kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye grigi ya Taifa.

Dar es Salaam. Mikoa inayopata huduma ya umeme katika gridi ya Taifa imekosa umeme kutokana na hitilafu iliyojitozea.

Hayo yamebainishwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutokana na hitilafu iliyojitokeza katika mfumo wa gridi ya Taifa leo asubuhi ya Desemba 4, 2024.

“Tunautaarifu umma kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika mfumo wa Gridi ya Taifa leo Disemba 4, 2024 majira ya saa 04:03 asubuhi, hitilafu hiyo imepelekea mikoa inayopata umeme katika gridi ya Taifa kukosa umeme,” imeeleza taarifa hiyo.

Tanesco imesema timu ya wataalamu inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu hiyo.

 Aidha, imeongeza kuwa umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha mikoa yote inapata umeme.

“Shirika linawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza, na litaendelea kutoa taarifa za hali ya urejeshaji wa huduma ya umeme kwa kadri hali inavyoimarika,” imehitimisha taarifa hiyo.


Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi.