Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tamasha kuhamasisha kilimo hai kufanyika Z’bar

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Maliasili, Shamata Shaame akizungumza kuhusu tamasha la kuhamasisha kilimo hai litakalofanyika Zanzibar Septemba 25 mwaka huu. Picha na Jesse Mikofu

Unguja. Katika jitihada za kukuza na kuendeleza kilimo hai, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wa kilimo hicho wameandaa tamasha litakalofanyika kisiwani humo kwa siku tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 2, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Maliasili, Shamata Shaame amesema tamasha hilo la siku tatu, linatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika viwanja vya Dimbani Dole Agosti 25.

"Pamoja na Serikali kujielekeza kwenye kilimo kwa ujumla wake, lakini imejielekeza zaidi katika kilimo hai, tunategemea tamasha hili kuwa la aina yake kuzidi hata maonyesho ya sikukuu ya wakulima ya nanenane," amesema Shamata.

Waziri Shamata amewataka wakulima na wadau wengine ambao wanafanya kazi zinazofanana na kilimo hai kuhakikisha wanajiandikisha mapema ili wapate fursa hiyo ya kipekee kwani ni mara ya kwanza kufanyika tamasha kama hilo siyo tu Zanzibar, lakini Tanzania kwa ujumla.

Amesema hiyo ni njia ya kuhamasisha wananchi kujihusisha na kilimo hicho ambacho kinamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kujenga afya imara na kuepusha magonjwa kutoka na kemikali.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na uwekezaji, Mudrick Soraga amesema kilimo hai sio tu kinajenga afya, pia kinaongeza ajira hivyo hatua hiyo ni kwenda sambamba na mpango wa Serikali wa kukuza uchumi na uwekezaji.

"Sasa kisiwa chetu kinaelekea mwelekeo wa kuwa na masuala ya kilimo hai, ikiwa ni sehemu ya kuinua hali za lishe za wananchi wetu, uchumi wa nchi yetu ni imani kubwa kuona jukwaa hili linakuwa chachu kutoa msukumo mkubwa na kuondoa dhana ya kwamba kilimo hai watu watakufa njaa na badala yake watu waone kuwa ni fursa zilizomo ndani na nje ya nchi na masuala ya mazingira," amesema

Amesema katika mabala ya Amerika na Ulaya, Serikali zinatumia mabilioni ya Dola kuwainua wakulima wao kuelekea katika kilimo hicho hivyo na Zanzibar ina fursa ya kipekee kuona inanufaika na kilimo hicho.

Tamasha hilo limeratabiwa na wadau wa kilimo hai wakiongozwa na Taasisi ya Kilimo Endelevu (PPIZ).

Mkurugenzi Mtendaji wa PPIZ, Ikram Soraga amesema kuna changamoto ya lishe na tamaduni kupotea hivyo wameumua kuleta tamasha hilo kuona jinsi ambavyo linawezakufanyika na kuleta hamasa kwa wananchi.

"Tunataka jamii ijue kuwa kuna fursa na mambo mengi, hili halijawahi kufanyika, kwahiyo ni fursa kiutalii na nchi yetu kujiweka katika soko la dunia kiushindani wa chakula kama tunavyojua kwasasa mataifa mengi yanatumia bidhaa ambazo hazina kemikali," amesema.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimo Endelevu, Dk Mwatima Juma amesema kuna fursa endelevu katika kilimo hicho na kwamba ndoto yake tangu zamani ilikuwa ni kukiona kisiwa hicho chote kinatumia kilimo hai.

“Mwendo ni hatua, hii leo ni hatua kubwa kueleka huko, tunapozungumzia kilimo hai tunaona kuna haja kubwa kwenye vipodozi tunataka view vya kiasilia, vyakula na mavazi vitokane na uasilia kwasbabu ya kulinda afya zetu,” amesema.

Katika tamasha hilo litakaofanyika kuanzia Agosti 25 hadi 27, litahusisha wasanii mbalimbali akiwemo Khadija Kopa, Rico single, Mzee Yusuph, Mrisho Mpoto na Ben Paul.

Baadhi ya wasanii hao Mzee Yusuf, Khadija Kopa na Rico kwa nyakati tofauti wamewahakikishia wananchi kwa siku hizo kutoa burudani kubwa itakayoambatana na elimu kuhusu kilimo.