Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takukuru yageukia rushwa ya ngono shule za msingi, sekondari

Muktasari:

  • Baada ya kukamilika kwa utafiti wa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu nchini, Takukuru imeegeukia shule ya msingi na sekondari.

Dar es Salaam. Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) imekamilisha utafiti wa viashiria vya rushwa ya ngono katika sekta elimu upande wa shule za msingi na sekondari kwa walimu.

Utafiti huo umefanyika ikiwa ni baada ya ule wa awali uliofanywa katika vyuo vikuu ikiwemo kile cha Dodoma (Udom) na Dar es Salaam (Udsm) uliofanyika mwaka 2019/2020 na matokeo yake kutangazwa.

Hayo yameelezwa katika maadhimisho ya miaka 15 ya mfuko wa Udhamini wa wanawake (WFT) yaliyofanyika jijini hapa yaliyohusisha wadau kutoka sehumu mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Akizungumza leo Februari 23, Mkurugenzi wa uzuiaji rushwa wa Takukuru, Sabina Seja amesema matokeo ya utafiti huo hutumika kuweka mikakati ya kudhibiti na kuzuia vitendo vya rushwa ya ngono.

Amesema katika utafiti uliofanywa kwa upande wa shule ya msingi tayari matokeo yake yamepelekwa kwa wahusika na sehemu zilizobainika kuwapo na mianya ya rushwa na viashiria vyake tayari wadau wameanza kuweka mikakati ya kushughulia suala hilo.

Utafiti huo umefanywa na Takukuru kwa kushirikiana na WFT ikiwa ni muendelezo wa kampeni maalumu ya kuvunja ukimya katika rushwa ya ngono na kuikataa.

"Tunatarajia kuwa kutakuwa na mabadiliko katika yale ambayo yameanza kutekelezwa na matokeo ya utafiti huu yatatumika kuweka mikakati katika maeneo ambayo yamebainika kuwa na vitendo vya rushwa pia kufanya kampeni ya vunja ukimya rushwa ya ngono haikubaliki," amesema.

Amebainisha kuwa wakati tafiti hizi zikifanyika, mwamko wa watu kuzungumzia juu ya rushwa ya ngono umeongezeka.

"Watu sasa wanaweza kufunguka au kujadili kihusu rushwa ya ngono au wafanye nini, kitendo cha rushw ya ngono kuweza kongeleka shuleni, vyuo hii jnamaana kuwa rushwa hii inaweza kuzuilika," amesema.

Sabina amebainisha kuwa licha ya kutofanya utafiti wa pili katika  katika chuo kikuu cha UDOM na UDSM ila kuna uimarikaji wa kuzuia rushwa hiyo hasa baada ya kuweka madawati ya kushughulikia malalamiko yaliyokuwapo.

Bila kutaja ni nani amenyooshewa kidole kwa kuomba zaidi rushwa katika tafiti hizo alisema kwa mujibu wa sheria wamekuwa wakijikita zaidi katika kutoa elimu na kuimarisha mifumo kuzia vitendo hivyo.

"Tunapofanya utafiti si lazima upate jina la mtu, likipatikana lazima uchunguzi ufanyike na ikithibitishwa anapelekwa mahakamani, tuzipopata jina tunatumia matokeo kuweka mikakati.

Wakati hili kikifanyika, Mkurugenzi wa WFT, Rose Marandu ameitaka serikali kukamilisha mchakato wa ubadilishaji wa sheria ya ndoa ili kuhakikisha hakuna mtu anaachwa nyuma.

Amesema Sheria hiyo kutoa mwanya wa watoto kuolewa chini ya miaka 18 kwa ridhaa ya inakatisha ndoto ya mabinti wengi.

"Unarudisha nyuma maendeleo yake, unarudisha nyuma maendeleo ya jamii, atapa mtoyo katika hmro usio sahihi, atashindwa kulea mtoto, mtoto hatokuwa productive katika jamii yake na ataendrlea kuishi katika umasikini hivyo ni wakati muafaka kwa bunge kuhakikisha sheria inabadilishwa.

Mfuko huu tangu kuanzishwa kwake mashirika 440 na zaidi watu 68,000 wameshanufaika na ruzuku zinazotolewa na mfuko huo.

Mfuko huo umekuwa ukitoa ruzuku kwa mashirika ya kutetea haki za wanawake, wasichana na watoto Tanzania unaoongozwa na itikadi ya fikra za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Theo Sowa aliyekuwa Mkurugenzi wa African Women's Development Fund (AWF) alisema ni muhimu kuwa na fedha zinazotumika kuchochea mabadiliko ya kimfumo na kutoa fursa muhimu zinazoleta mabadiliko katika harakati za wanawake katika bara la Afrika.

"Ni vizuri kuwapo na sera maalumu zinazohakikisha kuwa uwepo wa misaada ya kimataifa inatoa fursa na usawa katika kuongeza kiwango cha ruzuku kinachotolewa kuisaidia Afrika na jitihada za wanawake,” amesema Theo.