Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simanzi yatawala msibani kwa ndugu wanne waliofariki ajalini

Waombolezaji wakiwasili Mbezi Beach jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Dk Norah kuomboleza msiba wa ndugu wanne wa familia moja waliofariki ajalini Agosti 2, mwaka huu. Picha na Michael Matemanga.

Muktasari:

  • Waombolezaji wakusanyika kuomboleza msiba wa ndugu wanne wa familia moja waliofariki katika ajali iliyotokea usiku wa Agosti 2.

Dar es Salaam. Simanzi imetawala nyumbani ambako unafanyika msiba wa ndugu wanne wa familia moja waliopoteza maisha katika ajali iliyotokea wilayani Chalinze usiku wa Agosti 2.

 Wanafamilia hawa Sia Msuya, Neech Msuya, Dk Norah Msuya na Diana Msuya walipata ajali wakiwa safarini kuelekea msibani wilayani Same.

Tayari miili yao imewasili jijini Dar es Salaam na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo ikisubiri taratibu za maziko.

Baadhi ya wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika Mbezi Beach jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Dk Norah ambaye alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Mume wa Dk Norah, Dk Daud Momburi amesema kwa sasa hakuna taratibu yoyote inayoendelea kabla ya kufanyika kikao cha familia zote kinachotarajiwa kufanyika baadaye leo.

“Siwezi kusema chochote kwa sasa hadi kikao cha wanafamilia wote kikae, mimi ni mkwe itakuwa siyo vyema nikazungumzia msiba wote, tutakuwa na tamko la pamoja,” amesema Dk Momburi.

Miongoni mwa waombolezaji waliopo nyumbani hapo ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Makini waliofika  kumfariji Chloe Momburi ambaye ni mwanafunzi mwenzao na mtoto wa Dk Norah.

Marehemu Dk Norah ameacha watoto wawili wa Cleya na Chloe ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano.