Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi wa benki, mhadhiri wa Mzumbe wafariki dunia ajali Bagamoyo

Muktasari:

  • Ajali ya gari, iliyotokea jana Jumatano usiku katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, imepoteza maisha ya Mkurugenzi wa Benki ya ABSA na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Ajali ya gari, iliyotokea jana Jumatano usiku katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, imepoteza maisha ya Mkuu wa Kitengo cha majanga wa Benki ya ABSA na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 3, 2023 na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutuma.

Katika taarifa hiyo, imesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Agosti 2, saa 2:30 usiku, ikihusisha gari aina ya Toyota Prado na Scania.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa gari ya Toyota Prado ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, na kwamba ilikuwa ikiendeshwa na Neechi Msuya, huku Scania ilikuwa ikitokea Arusha na kwamba iliendeshwa na Philipo Mtisi.

Taarifa hiyo iliwataja waliofariki kwenye jali hiyo kuwa ni Neechi Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45 hadi 50, Dayana Mageta, mfanyabishara na makazi wa Dar es Salaam anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45, Nora Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45 ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, na abiria wa kike ambaye jina lake halikufahamika na anakadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 35.

Polisi imeeleza chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda upande wa kulia kisha kogongana uso kwa suo na lori hilo.

“Miili ya marehemu imehifadhiwa Zahanati ya Lugoba kwa uchunguzi wa daktari na itakabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha Jeshi hilo la Polisi limetoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara kuchukua tahadhari na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kusababishwa na uzembe.

Pia limewatahadharisha madereva kuacha kutumia vileo wanapoendesha vyombo vya moto kwani imekuwa chanzo cha kusababisha ajali za barabarani.