Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shuhuda asimulia ajali iliyoua 17 Tanga wakisafirisha msiba

Muktasari:

Mwanafamilia aliyepoteza ndugu 14 na wengine 12 wakijeruhiwa ajalini Tanga, amesimulia alivyoshuhudia ajali hiyo ikitokea akiwa katika basi la nyuma.


Korogwe. Mwanafamilia aliyepoteza ndugu 14 na wengine 12 wakijeruhiwa ajalini Tanga, amesimulia alivyoshuhudia ajali hiyo ikitokea akiwa katika basi la nyuma.

Ajali hiyo ilitokea jana Ijumaa saa 4:30 usiku katika eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, Barabara ya Segera - Buiko.

Akizungumza na Mwananchi leo Februari 4, 2023, Mark Mrema ambaye marehemu aliyekuwa akisafirishwa ni baba yake mdogo amesema msafara wao ulianzia Mbezi jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Bochi ambapo walihifadhi mwili wa ndugu yao aliyefariki dunia Jumanne Januari 31, 2023

Amesema wao walikuwa basi la nyuma na lililopata ajali likiwa mbele yao, ila muda mfupi waliona likiyumba na kupata ajali.

“Ni mshtuko kwa wanafamilia, tulianza harakati za kuwaokoa wenzetu muda huouo, huku kukiwa hakuna msaada kwa muda huo, ila baada ya muda mfupi walifika wananchi wa maeneo ya jirani pamoja na polisi, shughuli ya kuokoa ilianza,” amesema Mark.

Amesema walikuwa wakisafirisha mwili huo kwenda Wilaya ya Rombo Mkuu eneo la Mokala ambapo mazishi walikuwa wanatarajia yafanyike leo Jumamosi Februari 4.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe Salma Sued  imetaja majina ya waliofariki kwenye ajali hiyo.

Waliofariki ni Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema, Godwin H Mrema, Yusuph Saimon, Zawadi Mrema, Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina  A Lamosa, Evelina Cosmas Mrema na watoto wawili (mtoto wa binamu na mtoto wa Julieth).