Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheikh Njalambaha aitaka jamii kulaani ukatili

Waislamu mkoani Mbeya wakiswali swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika leo Jumamosi Aprili 22, 2023 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Muktasari:

  • Swala ya siku kuu ya Eid El Fitri kimkoa imefanyika leo Jumamosi kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya, ambapo Waislamu kutoka maeneo mbalimbali mkoani humo wamekusanyika pamoja kwa ajili ya ibada hiyo.

Mbeya. Viongozi wa dini mkoani Mbeya wamesema mmomonyoko wa maadili, ukatili wa kijinsia na mapenzi ya jinsia moja siyo jukumu la Serikali pekee bali kila mmoja anapaswa kukemea na kulaani ili kuwa na Taifa imara.

Akizungumza leo Jumamosi, Aprili 22 kwenye swala ya ibada ya siku kuu ya Eid El Fitri iliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Sokoine jijini humo, Sheikh wa Mkoa huo, Msafiri Njalambaha amesema kwa sasa hali si shwari na lazima kila mmoja alaani vitendo hivyo.

Amesema kama tofauti na kupinga vitendo hivyo matokeo yake ni kuiharibu dunia nzima na kumchukiza Mungu na kuwaomba wananchi kwa ujumla kufichua na kupiga vita aina yoyote ya ukatili.

“Tuache tamaa ambazo wakati mwingine huchangia hali hii, tufanye kazi tukisubiri malipo kutoka kwa Mungu, ubakaji, ulawiti na mauaji na mapenzi ya jinsia moja yanazidi kulitesa dunia, tusiiachie Serikali pekee bali jamii nayo iungane kwa pamoja kulaani,” amesema Njalambaha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Maimamu mkoani humo, Sheikh Iddy Tuwa amewataka Waislamu kuendeleza matendo mema baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, akieleza kuwa vinginevyo ni kuharibu funga.

“Tulikuwa na kipindi chema ambacho kila mmoja wetu alifanya mambo mazuri, sasa isiwe ni mwisho baada ya mwezi huu mtukufu, tuendelee kushirikiana na kufanya yaliyo mema ya kumpendeza Mungu,” amesema Tuwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka Waislamu kusherekea kwa amani na upendo akisema kuwa kwa sasa jiji la Mbeya linaenda kubadilika kutokana na miradi ya maendeleo.

“Tupige vita ukatili wa kijinsia lakini niwaombe tuendeleze amani, upendo na mshikamano, jiji letu linaenda kubadilika kitaswila kutokana na miradi ya maendeleo inayoenda kufanyika ikiwamo barabara ya njia nne,” amesema Malisa.