Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shahidi aleza mke wa Bilionea Msuya alivyokamatwa Arusha na kusafirishwa hadi Dar

Muktasari:

  • Shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya na mfanyabiashara Revocatus Muyella, ameieleza Mahakama Kuu mshtakiwa Mrita alivyokamatwa Arusha na kusafirishwa kuja Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya na mfanyabiashara Revocatus Muyella, ameieleza Mahakama Kuu mshtakiwa Mrita alivyokamatwa Arusha na kusafirishwa kuja Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 103/2018 wakidaiwa kumuuwa kwa kukusudia Aneth Msuya, dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni, Dar es Salaam.

Kesi hiyo ndogo inatokana na mshtakiwa wa kwanza Miriam Mrita, kupinga maelezo yake ya onyo yasipokewe mahakamani kama ushahidi kwa madai kuwa aliteswa wakati wa kuchukuliwa maelezo hayo.

Shahidi huyo anayetoka Makao Makuu ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai, David Mhanaya (54) ameeleza hayo leo Desemba Mosi wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo ndogo.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Gloria Mwenda mbele ya Jaji Edwin Kakolaki, shahidi huyo amedai Agosti 4, 2016 alipokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Athumani Diwani kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Temeke.

Ameeleza baada ya kupokea maelekezo hayo aliondoka yeye na timu yake akiwemo ASP Jumanne, Lathifa Chiko, koplo Mwajuma pamoja na dereva Yahya.

Shahidi huyo ameeleza baada ya kufika kwa RCO Temeke walipewa maelekezo ya kwenda kuongeza nguvu kwenye tukio la mauaji ya Aneth Msuya yaliyotokea Kibada Kigamboni.

"Tulishirikiana na RCO kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kubadilishana taarifa za kiupelelezi, zilipatikana taarifa mtu aliyehusika na tukio hilo yuko Arusha, ambapo tulitakiwa mimi na timu yangu kufanya juhudi za kumpata," ameeleza shahidi huyo.

"Niliondoka na timu yangu akiwemo Lathifa, Jumanne, Yahya kwenda Arusha ambapo koplo Mwajuma alibaki na RCO kwa shughuli nyingine za kiupelelezi,"

Akiendelea na ushahidi wake Mhanaya amesema Agosti 4,2016 saa 5:30 usiku waliondoka kuelekea Arusha wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land cruse na kufika Agost 5, 2016 saa 3 asubuhi.

" Tuliwasiliana na Mkuu wa Upelelezi Arusha, SSP George Katabasi na kumueleza sababu za kwenda Arusha, aliuliza kama tungehitaji msaada lakini tulimwambia tungemjulisha kwani mtuhumiwa mwenyewe ni maarufu," ameeleza.

Shahidi huyo ameeleza kuwa wakati wanaendelea na upelelezi, ilipofika saa 12 jioni walipata taarifa kutoka kwa msiri  wao mtuhumiwa alikuwa Tembo Club barabara ya Monduli.

" Tuliondoka na gari hadi Tembo club na kukuta mtuhumiwa anakula, tulikaa pembeni na alipo maliza nilitoa maelekezo kwa Inspekta Lathifa kufanya ukamataji ambapo alimfuata na kukamata kisha kujitambulisha na kumueleza kosa lake.

Katika ushahidi wake, shahidi huyo ameiambia mahakama kuwa walifika katika makazi ya mtuhumiwa huyo na walimtafuta shahidi ambaye ni mjumbe Jacob Sibore na kuanza upekuzi.

Ameeleza kuwa katika upekuzi huo walikuta kadi nyingi za magari na kutaka kujiridhisha magari hayo yalipo kwani walipata taarifa kuwa baadhi ya magari mtuhumiwa alisafiri nayo hadi Dar es Salaam kutekeleza tukio.

"Nilimjulisha RCO na kuungana naye hadi kwenye hoteli yake inayoitwa SG, tuliyaona magari na kufanya ukaguzi kisha RCO akasema atafanya utaratibu wa kuyasafirisha hadi Temeke ambapo ndipo tukio lilipotokea,"

"Agosti 6,2016 saa 12 asubuhi safari ya kurudi Dar ilianza kwa mwendo wa kawaida, tulipofika Korogwe tulipata chakula kisha safari ikaendelea na kufika kituo cha polisi Teme saa tatu usiku, Nilimjulisha RCO SSP Mchomvu alielekeza tupumzike hadi siku inayofuata.