Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh500 milioni zatengwa kwa wakulima wa mbogamboga na matunda

Mbeya. Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Ushirika imetenga zaidi ya Sh500 milioni kwa ajili ya kusaidia wakulima wa mbogamboga na matunda ili kusaidia kundi hilo.

Hadi sasa tume hiyo imefikia mikoa saba ambayo ni Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Manyara, Arusha na Kilimanjaro ikitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Mratibu wa mafunzo kutoka Tume ya Taifa ya Ushirika, Deogratias Bendera amesema hayo jijini hapa kuwa mafunzo hayo yalilinga katika kujifunza matumizi ya fedha pamoja na kuwajengea uwezo ya jinsi ya kupata masoko, mitaji, sehemu za kuhifadhia mazao na utunzaji wa mahesabu.

"Zaidi ya Sh500 milioni imetengwa kwaajili ya kutoa mafunzo kwa vyama vya ushirika vya mbogamboga na matunda ambavyo vina mchango mkubwa sana kwa jamii sababu sehemu kubwa wao ndio wanaoendesha maisha ya watu.

"Unapokuwa kwenye ushirika kuna faida nyingi hata katika upangaji wa bei na kutafuta soko inakuwa njia nyepesi sababu mnakuwa katika mfumo mzuri unaotambulika," amesema Bendera

Mwenyekiti wa kikundi cha Kilimo na Lishe Mbeya Jiji, Maria Washaha amesema mafunzo hayo yamewasaidia sehemu kubwa kama viongozi wa vikundi hasa katika mfumo wa kuhifadhi fedha.

"Nimejifunza namna ya kutafuta masoko, kuhifadhi fedha pia mbinu ambazo wengine hutumia katika vikundi vyao hasa jinsi ya kuwafanya wakulima kujiunga na vikundi hivi."

Mwenyekiti UWAVIMAMBO Rungwe, Baraka Mwakatobe alisema mara nyingi viongozi wa vikundi kama hivi huendeshwa kwa kutumia akili ya kuzaliwa lakini mwisho wa siku serikali imewakumbuka.

"Serikali imeona umuhimu wetu ndio maana imeamua kuweka nguvu huku kwa kutoa fedha na mafunzo ili uzalishaji uwe mkubwa na uliobora zaidi."

Ofisa utumishi Mkoa wa Mbeya, Donald Bombo amesema kuna fursa nyingi kwenye kilimo na inapswa kuchangamiwa haraka ili kukimbizana na soko lilivyo.

Alisema kilimo hutoa ajira kwa watu wengi na wengi wametajirika kupitia sekta ya kilimo kwa kuwekeza na kusimamia ipasavyo hivyo serikali ipo karibu zaidi na wakulima.