Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh120 bilioni kusafirisha gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba Mtwara

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame (katikati) akisaini mkataba na Mkandarasi Mkuu (CPP & CPTDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Uongozi ya (CPP), Bai Zhengshuai (kushoto) na mwakilishi wa kampuni ya CPTDC, Li Haisheng kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba jijini Dar es Salaam leo. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Ni gesi asilia ambayo haijachakatwa na lengo ni kuongeza kiwango cha gesi kinachochakatwa katika kiwanda cha gesi Madimba mkoani Mtwara.

Dar es Salaam. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema litatumia takribani Sh120 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la gesi asilia kutoka Kijiji cha Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara.

Kauli hiyo ya TPDC imetolewa leo Julai 3, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mussa Makame katika hafla fupi ya kuingia makubaliano ya ujenzi wa bomba hilo.

Makubaliano hayo ni baina ya TPDC na  Kampuni ya China ya  Petroleum Pipeline Engineering (CPP) na China Petroleum Technology and Development Corporation (CPTDC) kwa kipindi cha miezi 12.

"Bomba litakalojengwa litakuwa na  inchi 14 na uwezo wa kusafirisha gesi ya futi za ujazo milioni 140 kwa siku, kiwango hiki cha gesi kina uwezo kuzalisha umeme wa megawati 700,mradi huu  ni muhimu kwa watumiaji gesi asilia,

Gesi ya Mnazibay na Songosongo zimekuwa za muda mrefu, Songosongo imezalisha gesi kwa miaka 20, Mnazibay miaka 18 na kiwango cha gesi kimeshaanza kupungua hivyo tunahitaji vyanzo vipya," amesema.

Makame amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa Bomba kazi itakayofanywa na TPDC na kazi ya uchimbaji wa visima itafanywa na Kampuni ya ARA Petroleum kazi ambayo itakamilika kwa miezi 12.

Katika utekelezaji wa ujenzi wa bomba hilo, Makame amesema vijiji 11 vitapitiwa na mradi huo na tayari tathmini ya mazingira imefanyika pamoja malipo ya fidia kwa watakaopitiwa na mradi.

Mkurugenzi Mtendaji wa CPP ya China, Bai Zhengshuai amesema mradi huo wataukamilisha kwa wakati na watazingatia Sheria za nchi wakati wa ujenzi wa bomba hilo.

"Mradi huu tutautekeleza kwa wakati na tutafuta sheria za nchi, mradi huu kwetu tutaufanya kwa ufanisi ili kuendeleza ushirikiano wetu," amesema.


Kuhusu gesi asilia

Tanzania inakadiriwa kuwa na mita trilioni 230 za ujazo za gesi asilia, ingawa zilizothibitishwa mpaka sasa ni futi trilioni 57.5, hivyo kuiweka kwenye ramani ya dunia ikishika nafasi ya 82.

Gesi hiyo tayari imeanza kuchimbwa katika visiwa vya Songosongo mkoani Lindi  na eneo la Msimbati mkoani Mtwara, ikitumika kuzalisha umeme na kuendesha mitambo ya baadhi ya viwanda nchini, majumbani na kwenye magari.