Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kuwalipa wananchi Kipunguni Dar Sh143.9 bilioni

Wakazi wa Mtaa wa Kipunguni Kata ya Kipawa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kusikiliza kuhusu hatima yao ya fidia baada ya kutakiwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.

Muktasari:

  • Kilio cha muda mrefu cha wakazi wa mtaa wa Kipunguni Kata ya Kipawa waliotakiwa kuhama eneo hilo kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege, kimefikia tamati baada ya Serikali kutangaza kuanza kulipa kufuatia kukamilika kwa tathmini.

Dar es Salaam. Kiasi cha Sh143.9 bilioni kinatarajiwa kutumika kulipa fidia wakazi wa mtaa wa Kipunguni kata ya Kipawa ili wapishe upanuzi wa uwanja wa ndege.

Fedha hizo zitatolewa baada ya kukamilika kwa tathmini mpya iliyoanza kufanyika Julai mwaka jana ambayo imeonyesha kuwa jumla ya watu 1865 wanatakiwa kupata fidia hiyo.

Leo Julai 7 Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba alitangaza kukamilika kwa taratibu zote za tathmini na kueleza kuwa tayari Serikali imesharidhia kulipa fidia hiyo kinachoendelea sasa ni hatua za ndani kabla ya watu kuanza kulipwa.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kipunguni, Dk Nchemba ameeleza kuwa tayari ofisi yake imepokea barua ya tathmini na kinachoendelea sasa ni kukamilisha taratibu za ndani ili malipo yaanze kufanyika.

“Tunawashukuru kwa uvumilivu huu, mmekuwa kielelezo cha Watanzania wazalendo na wanaojali maendeleo ya nchi. Tumeshapokea barua inayoonyesha tathmini imeshafanyika hivyo mnakwenda kulipwa fedha zenu.

“Tunafahamu mwaka mpya wa fedha ndio umeanza, tunakwenda kulifanyia kazi ndani ya robo ya kwanza ya mwaka na katika kipindi hicho itatolewa tangazo la tarehe rasmi ya lini mtaanza kulipwa,” amesema Nchemba.

Kwa upande wake Mbunge wa Segera Bona Kamoli amesema uamuzi huo wa Serikali umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu na wakazi wa eneo hilo hasa baada ya kuishi kwenye umaskini mkubwa.

“Hili suala nimelipigia kelele kwa muda mrefu tangu nimeingia bungeni, hawa wananchi tangu waliambiwa awataondoka hapa wamekuwa wakiishi kwa kubahatisha.

“Walishindwa kuendeleza makazi yao matokeo yake nyumba nyingi za huku zimechakaa, walikuwa wanashindwa hata kuanzisha biashara wakihofia kubomolewa, tunashukuru tunaenda kulihitimisha,” amesema Bona.

Mbunge huyo alisema ni imani yake kuwa mkutano huo ndiyo utakuwa wa mwisho baada ya kukaa mikutano mingi ya aina hiyo kwa ajili ya wananchi kudai fidia.

“Wananchi wanataka wapate fedha zao, suala la viwanja watakutana nalo mbele kwa mbele, tunaomba fedha zao zilipwe kwa haraka ili waondoke hapa maendeleo yafanyike maana kuna wananchi wengine watabaki hivyo eneo hili linahitaji kuendelezwa zikiwemo barabara,” amesema Bona.

Mwaka 1995 Serikali ilitangaza kulichukua eneo hilo kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege na miaka miwili baadaye ilifanyika tathmini, hata hivyo katika kipindi chote hicho hakuna malipo yaliyofanyika.