Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia: Mchakato Katiba mpya kufanyiwa kazi

Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa, suala la Katiba mpya linakwenda kufanyiwa kazi ndani ya miaka mitano ijayo.

Amesema kwa kuwa suala la Katiba ni pendekezo la muda mrefu la tume ya maridhiano, pendekezo hilo litafanyiwa kazi kama inavyoelekezwa na Ilani ya CCM.

“Kwa msingi huo, mchakato wa Katiba mpya ni miongoni mwa ahadi zinazoonekana katika Ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030. Hivyo ni kusema kwamba, shughuli ya kuanza kufanya Katiba mpya itatekelezwa katika kipindi kijacho cha miaka mitano,” amesema.

Rais Samia amesema hayo leo Juni 27, 2025 bungeni jijini Dodoma alipolihutubia kuhitimisha shughuli za Bunge la 12.
Mchakato wa Katiba mpya ulianza mwaka 2011 kwa utungwaji wa sheria za kuratibu na kusimamia utekelezaji wa upatikanaji wake. 

Sheria hizo ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83/2011 iliyoelekeza kuundwa vyombo vya kuratibu mchakato wa Katiba, yaani Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalumu la Katiba (BMK) na Sheria ya Kura ya Maoni Namba 11/2013.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba iliratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba iliyohaririwa na Mabaraza ya Katiba na kupata Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa kwenye BMK.

Katika Bunge hilo ambalo licha ya mvutano wa kiitikadi wa wajumbe uliosababisha baadhi ya wajumbe kususia majadiliano na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), lilijadili na Oktoba 2, 2014 lilipitisha Katiba pendekezwa.

Oktoba 8, 2014, aliyekuwa mwenyekiti wa BMK, Samwel Sitta aliikabidhi Katiba pendekezwa kwa Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete.

Hata hivyo, Aprili 2, 2015 ilitangazwa kuahirishwa kura ya maoni ya Katiba pendekezwa