Samia awataka wanaume kumuinua mtoto wa kike

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Muktasari:
- Samia ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti Club iliyofanyika sambamba na harambee ya ‘fadhili mtoto asome’ inayolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa Wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika la Binti Foundation.
Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NGO) kujenga utamaduni wa kuwashirikisha wanaume katika kampeni za kumuinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.
Samia ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti Club iliyofanyika sambamba na harambee ya ‘fadhili mtoto asome’ inayolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa Wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika la Binti Foundation.
Amesema wanaume kama mawakala wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika kuzungumzia umuhimu wa kumuinua mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala ya ujasiriamali.
"Penye mkusanyiko wa watu 100, ukiingiza wanaume 20 na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu, wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje," amesema.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz