Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la Mwabukusi, Mpoki laamsha moto

Dar es Salaam. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimesema hakijaridhishwa na uamuzi wa Kamati ya maadili ya Mawakili wa kumsimamisha kazi kwa miezi sita wakili wa kujitegemea, Mpale Mpoki na kimechukua hatua kadhaa, ikiwemo ya kuondoa wajumbe wake katika kamati hiyo.

TLS pia imemwongeza wakili Stevephen Mwakibolwa katika timu ya mawakili wanaomtetea Boniface Mwabukusi mbele ya kamati hiyo na ikijiandaa kukata rufaa.

Katika shauri hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Eliezer Feleshi amemfikisha wakili Boniface Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili kwa kile kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu, zikiwamo kauli zake za kupinga makubaliano ya uwekezaji katika bandari alizotoa hivi karibuni.

Mbali na Mpoki, Baraza la Utawala la TLS lilimemteua wakili Dk Rugemeleza Nshala kuwa miongoni mwa wanaomtetea Mwabukusi.

Shauri hilo lililosikilizwa juzi Novemba 20, lilishindwa kuendelea baada ya kutokea mabishano ya kisheria yaliyosababisha wakili Mpoki kusimamishwa na kamati hiyo kwa miezi sita.

Juhudi za Mwananchi kumtafuta Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji Ntemi Kilekamajenga, kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa, lakini Katibu wa kamati hiyo, Faraji Ngukah alikiri kuwa Mpoki amesimamishwa kwa muda huo na kwamba yupo kwenye kikao, hawezi kuzungumzia zaidi.

"Ni kweli Mpoki amesimamishwa na mimi nipo kwenye kikao cha kamati, hivyo siwezi kuongea zaidi maana vikao vinaendelea," alidai Ngukah na kukata simu.


Tamko la TLS

Taarifa iliyotolewa jana na Rais wa TLS, Harold Sungusia imesema kuwa wakili huyo alisimamishwa baada ya kutaka kuweka mapingamizi wakati shauri hilo linaendelea kusikilizwa na kamati na kwamba Mpoki amehukumiwa bila kusikilizwa.

“Mpoki amelieleza Baraza la Utawala kwamba, wakati wa kusikiliza kesi ya Mwabukusi Novemba 20, 2023, aliibua hoja za mapingamizi ya awali. Awali Mwenyekiti hakutaka kuendelea na mapingamizi hayo akionya kwamba hafurahishwi na mapingamizi,” imesema taarifa hiyo.

“Hakupewa hata nafasi ya kusikilizwa na zaidi hakuna kifungu kinachompa mamlaka mwenyekiti kumwondoa wakili anayewakilisha upande katika kamati hiyo.”

Kutokana na hali hiyo, TLS imesema itachukua hatua ya kuwaondoa wajumbe wake katika kamati hiyo kuanzia jana hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

“Baraza la Utawala linamteua mjumbe wake Stephen Mwakibolwa kuungana na timuy ya mawakili ili kumwakilisha Mpiki ikiwa pamoja na kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa kumwondoa Mpoki.

“Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwanachama wake, TLS inapaswa kufungua madai dhidi ya Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga J mbele ya Tume ya Majaji ukatili kwa mawakili kiwasi kwamba wote walijitoa kwenye kesi hiyo,” imesema.

Mbali na taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Mawakili Vijana kutoka Kutoka TLS, Edward Heche alisema sheria hazikufuatwa kikamilifu kwa sababu wakati uamuzi unafanyika, mwenyekiti wa kamati hana nguvu ya kumsimamisha wakili, bali hiyo nguvu anayo jaji wa Mahakama Kuu.