Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za utoro wanafunzi Geita zatajwa

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo akikabidhi kitabu cha muongozo uboreshaji elimu kwa shule za msingi na sekondari kwa afisa elimu kata Mary Kavula.

Muktasari:

Shughuli za kiuchumi ikiwemo uchimbaji mdogo wa dhahabu,kilimo na uvuvi vimetajwa kuchangia utoro kwa wanafunzi wa shule za msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Geita hali inayosababisha halmashauri hiyo kufanya vibaya katika mitihani ya Taifa.

Geita. Shughuli za kiuchumi ikiwemo uchimbaji mdogo wa dhahabu, kilimo na uvuvi vimetajwa kuchangia utoro kwa wanafunzi wa shule za msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Geita hali inayosababisha halmashauri hiyo kufanya vibaya katika mitihani ya Taifa.

 Kwa mujibu wa afisa elimu msingi wa halmashauri hiyo, Edith Mpinzile amesema wanafunzi 10,000  kati ya 48,000 wa darasa la nne na wanafunzi 2,000 kati ya 19,000 wa darasa la saba mwaka 2021 hawakufanya mtihani wa taifa mwaka 2021.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu vya miongozo na uboreshaji elimu kwa shule za msingi na sekondari, Mpinzile amesema hali ya utoro kwa halmashauri hiyo ni mbaya.

Amesema changamoto nyingine ni muamko mdogo wa elimu kwa wazazi, upungufu wa walimu na umbali wa shule vimechangia wanafunzi kuwa watoro.

Mbali na utoro wa wanafunzi pia amesema upo utoro wa walimu ambapo baadhi licha ya kufika shuleni lakini hawaingii darasani kufundisha hivyo kuathiri ufaulu kwa wanafunzi na kusema miongozo iliyotolewa na serikali itasaidia kuleta mabadiliko.

Kutokana na hali ya utoro, Mkuu wa wilaya ya Geita, Wilson Shimo amewataka watendaji wa vijiji na maafisa elimu kata kuwachukulia hatua wazazi wanaoshindwa kuwajibika kwa watoto wao kutohudhuria shuleni na kujiingiza kwenye shughuli za kiuchumi.

“Uzembe kwa wazazi na wanafunzi kushindwa kuwajibika upo utoro wa rejareja ambao tunasema sio mbaya lakini mimi niseme ni mbaya viongozi chukueni hatua ili kupunguza utoro kwa wanafunzi wetu,” amesema

“Nimetembelea shule ya msingi Saragurwa nimekuta wanafunzi zaidi ya 300 ni watoro yani siku moja watoto 300 hawajafika shule nimeenda kwenye shule ya Sanza kijiji hichohicho watoto zaidi ya 400 hawajafika shule watoto 700 wanazurura kijijini wazazi,viongozi wapo hawawajibiki “amesema Shimo

Kaimu afisa elimu wa halmashauri hiyo, Dk Modest Burchard amewataka walimu wakuu na maafisa elimu kata kuacha kutumia changamoto zilizopo shuleni kama kichaka cha wao kutowajibika.