Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saba wafariki, 22 wajeruhiwa ajali ya basi

Muktasari:

  • Watu saba wamefariki dunia na 22 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea eneo la Kiwawa katika Halmashauri ya Kilwa, mkoani Lindi.

Kilwa. Watu saba wamefariki dunia na 22 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria eneo la Kiwawa katika Halmashauri ya Kilwa, mkoani hapa.

 Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Oktoba 06, 2023; Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, ACP Pili Mande amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 8 mchana.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, Scania ni mali ya kampuni ya Saibaba linalofanya safari zake kati ya Nachingwea na Dar es Saalam na Tata ni ya kampuni ya Baharia, ambalo linafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tandahimba mkoani Mtwara.

ACP Mande ameendelea kusema kuwa kwenye ajali hiyo madereva wa magari yote wamefariki papo hapo, huku akiwataja kwa majina kuwa ni dereva wa basi la Saibaba Lucas John (59), Mkazi wa Arush, na mwenzie wa kampuni ya Baharia Omary Abdalla (47), Mkazi wa Dar es Salaam.

"Waliofariki papo hapo ni madereva wawili pamoja na abiria watano ambao miili yao bado haijatambuliwa hadi sasa, na miili imehifadhiwa katika Hosptali ya Kinyonga iliyopo wilayani Kilwa mkoani Lindi," amesema Kamanda Mande.

Bosi huyo wa Polisi mkoani Lindi amesema kuwa majeruhi watatu kati ya 22, hali zao ni mbaya, na kwamba japo majina yao hayajafahamika, ila wapo wanawake wawili na mtoto mmoja wa kiume, na kwamba wote wamelazwa katika hosptali hiyo.

Kwa upande mwingine RPC huyo amesema kuwa majeruhi wengine 19 wanaendelea kutibiwa na kuangaliwa afya zao kama wataendelea vuzuri wataruhusiwa.

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo, Kamnda Mande amesema: “Chanzo cha ajali ni dereva wa basi la kampuni ya Saibaba kutaka kulipita gari kubwa la mizigo ambalo lilikuwa mbele yake na ndipo alikutana na basi hilo dogo la kampuni ya Baharia likitokea Dar es Salaam na kugongana uso kwa uso.”

Aidha Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Wilaya ya Kilwa, Lusajo Mwakajoka amekiri, kupokea majeruhi 22, ambapo amesema kati yao wanawake ni 11; huku miili saba ikipokelewa ambayo ni ya wanaume wanne na  mwanamke 1  na watoto wawili ambayo bado imehifadhiwa hosptalini hapo.

Hata hivyo amesema kutokana na hali za wajeruhi na watatu na mtoto mmoja, “wamepelekwa Hosptali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi."

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa madereva wote kufuata sheria za usalama barabarani na kuwa makini na kipindi mvua inapokuwa inanyesha kwa kuwa barabara inakuwa inateleza.