Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia azindua miradi Kizimkazi

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

Kilele cha Tamasha la Kizimkazi, wilaya ya Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar litahitimishwa kesho Jumamosi huku leo Ijumaa, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo la Kizimkazi wilaya ya Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Sehemu kubwa ya miradi hiyo ambayo ameizindua leo Ijumaa, Septemba 2, 2022, imetekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi za fedha ikiwa ni kuelekea kilele cha tamasha la Kizimkazi ambalo hufanyika kila mwaka na litahitimisha kesho Jumamosi.

Mradi wa kwanza aliozindua ni wa maabara ya sayansi katika sekondari ya Kizimkazi ambayo imejengwa kwa msaada wa benki ya CRDB.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema lengo la benki hiyo ni kuona vijana wanasoma katika mazingira ya kisasa kuendana na kasi ya teknolojia na ndiyo sababu imejikita kusaidia eneo la elimu.

“Tunataka kuwa sehemu ya kuandaa watalaam ambao watatusogeza mbele kama taifa, kufanikisha hilo ni lazima tuwe na mchango katika elimu na ndiyo maana leo tumewezesha hapa kuwa na maabara itakayosaidia kupata wanasayansi,” amesema Nsekela.

Aidha, Rais Samia amezindua ofisi za chama cha ushirika Kizimkazi ambacho samani zake zimewekwa na benki ya NBC.