Rais Samia atunukiwa shahada ya heshima Russia, asema ni ya Watanzania wote
Muktasari:
- Rais Samia ameelekeza shahada hiyo ya heshima kwa Watanzania wote akisema kuwa ni mchango wao katika maendeleo ya Taifa na kimataifa.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) jijini Moscow, Russia, huku akisema heshima hiyo si ya mafanikio yake binafsi bali ni utambuzi wa mchango wa Watanzania wote katika maendeleo ya Taifa na ushirikiano wa kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Russia- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Russia, Juni 4, 2026.
Shahada hiyo ametunukiwa leo Alhamisi Juni 4, 2026, wakati wa ziara yake ya kitaifa nchini Russia, ambapo uongozi wake, mchango katika maendeleo ya kijamii, mageuzi ya elimu na diplomasia ya kimataifa vimetajwa kuwa sababu za kutambuliwa kwake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Russia- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Russia, Juni 4, 2026.
Hafla ya kutunukiwa shahada hiyo imefanyika chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kitaifa nchini Russia.
Akizungumza baada ya kutunukiwa shahada hiyo, Rais Samia amesema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Russia- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Russia, Juni 4, 2026.
"Shahada hii haihusu mafanikio yangu binafsi, bali ni utambuzi wa mchango wa Watanzania wote katika maendeleo ya Taifa na ushirikiano wa kimataifa. Naipokea kwa upole, kama Rais wa Tanzania, mtoto wa Afrika na rafiki wa Russia. Siipokei kwa ajili yangu, bali kwa ajili ya Watanzania."
Rais Samia ameongeza kuwa tuzo hiyo inakumbusha umuhimu wa elimu na maendeleo ya watu kama msingi wa uongozi bora.
Akizungumza baada ya kumtunukia shahada hiyo, Profesa Oleg Yastrebov, mhadhiri wa chuo hicho, amesema Rais Samia amekuwa na mchango mkubwa katika uongozi, maendeleo ya kijamii, mageuzi ya sekta ya elimu, diplomasia ya kimataifa na kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Russia- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Russia, Juni 4, 2026.
Kutunukiwa kwa heshima hiyo kunafanya idadi ya shahada za heshima za Rais Samia kufikia nane, kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania.