Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia atoa maelekezo Tume ya Mipango

Rais Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

  • Julai 5, 2023, Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Wizara ya Nchi katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na alimteua mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo kuiongoza wizara hiyo mpya

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Julai 5, 2023 baada ya kubadilisha muundo wa wizara mbili na kuunda wizara mpya ya Mipango na Uwekezaji pamoja na Tume ya Mipango.

Vilevile, Rais Samia amewaapisha makamu mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na baada ya viapo vya kazi, viongozi na watendaji hao walipewa kiapo cha maadili ya watumishi wa umma.

Walioapisha leo Julai 14, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba na naibu wake, Hamad Chande, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji na naibu wake, Exaud Kigahe na Profesa Kitila Mkumbo anayekwenda Wizara ya Mipango na Uwekezaji.

Wengine ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Laurence Mafuru na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha, Elijah Mwandumbya

Vilevile, Rais Samia amemwapisha Makamu Mwenyekiti wa Nec, Mbarouk Salim Mbarouk, wajumbe wa Tume hiyo, Omar Mapuri, Zakia Mohamed Abubakary.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao, Rais Samia aliwapongeza na kutoa maelekezo mahsusi kwa Tume ya Mipango kwenda kutafuta vichwa vizuri vitakavyosaidia kufikiri na kupanga maendeleo ya nchi hii.

“Kama mnaweza kutafuta vichwa makini vyenye uzalendo, hii ndiyo inakuwa think tank (wanaofikiria) ya Tanzania kwa sababu mipango iko hapo, TR (Msajili wa Hazina) anayechunga mali zetu yuko hapo lakini pia uwekezaji uko hapo,” amesema.

Rais Samia amesema wanakosolewa huko mitandaoni baada ya kuamua na kupanga lakini kama wanaona watu wazuri huko nje, wawachukue ili wawe sehemu ya Tume ya Mipango, wakafikiri pamoja na ili tuondoa vuguvugu kwamba wamepanga nini.

“Kwa hiyo, kila mnayehisi anaweza akasaidia, leteni list tuone, tuwafanyie vetting vizuri, tuwaweke kwenye Tume ya Mipango. Tanzania ni yetu wote, wote tufikiri, tukawaze kwa ajili ya nchi yetu,” amesema.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amempongeza Rais Samia kwa kuirudisha Tume ya Mipango kwa sababu maendeleo endelevu ya hayatokei ghafla bila kupangwa, ujenzi wa nchi ni matokeo ya juhudi za kujenga nchi.

Amempongeza Mafuru kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, hata hivyo alisema ana kazi kubwa tatu ambazo ni kubainisha hali halisi ya maendeleo ya nchi, kubadilisha mwelekeo wa nchi kimkakati na kuongoza maandalizi ya dira ya Taifa ya mwaka 2050.

“Ukaongoze ufanyaji wa hizo kazi kwa kushirikiana na wizara zote na kwa msisitizo, ukashirikiane sana na sekta binafsi lakini pia chama tawala (CCM), Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Fedha na wizara nyingine,” amesema Dk Mpango.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema anaamini kwa ahadi wazizozitoa zitabaki ndani ya mioyo yao na watakwenda kuzifanyia kazi na kwamba Mahakama ya Tanzania itatoa ushirikiano kwao.