Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua bosi mpya Usalama wa Taifa

Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa leo Agosti 28, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Rais aigusa tena Idara ya Usalama wa Taifa kwa kufanya mabadiliko katika uongozi wa juu baada ya aliyekuwepo kuteuliwa kuwa balozi.

Dar es Salaam. Ikiwa imepita takribani miezi nane tangu Said Hussein Massoro ateuliwe kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan leo amefanya mabadiliko

na kumteua Balozi Ali Idi Siwa katika nafasi hiyo.

Massoro aliteuliwa kushika nafasi hiyo Januari 3 mwaka huu na kudumu kwenye ofisi hiyo nyeti kwa miezi nane kabla ya kuteuliwa kuwa balozi.

Kabla ya kupewa jukumu hilo Massoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Balozi Siwa ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam tayari kuitumikia nafasi hiyo nyeti na muhimu kwa Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Siwa alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko

wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) nafasi aliyohudumu tangu Septemba 20, 2018.

Kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda kwa takribani miaka mitatu kuanzia 2015 hadi 2018.