Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ataka demokrasia iboresha maisha ya wananchi

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kabla ya kufungua Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha Julai 17, 2023.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amesema lazima demokrasoa iwe njia ya kuwaunganisha wananchi.

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili demokrasia iwe na maana kwa maisha ya wananchi ni lazima ilete matokea katika huduma muhimu za jamii na kuboresha maisha wananchi.

 Amesema demokrasia lazima iwe njia thabiti iliyodhibitishwa kuwaunganisha wananchi. 

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 17, 2023 jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa wadau wa Demokrasia Afrika, ambao utahusisha viongozi wakuu wastaafu wa Afrika.

 “Serikali kushindwa kutoa huduma kwa wananchi ndio sababu ya kuanzisha kwa mifumo ya kuwasilisha mahitaji ya wananchi kama uwepo wa wanaharakati, maandamano kushinikiza upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi na hapa ndipo uhuru wa kujumuika na kutoa maoni unapotumika tofauti,”amesema.

 Rais Samia amesema haoni mbadala wa demokrasia kama nchi za Afrika hazitakuwa na mikakati ya kuwa na maendeleo endelevu na uchumi imara akisisitiza demokrasia ina uhusiano mkubwa na masuala ya aamani na ukuaji wa kasi wa uchumi.

Katika kuaenzi miaka 30 ya vyama vingi nchini, Rais Samia amesema ameanzisha  R nne ambazo ni maridhiano (Reconciliation), mabadiliko (Reforms), ustahimilivu (Resilience) na kujenga upya (Rebuilding) lengo kuu lilikuwa kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahimilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu.

Amesema kupitia R4 tayari Serikali imepokea ripoti ya haki jinai na sasa ipo kwenye hatua ya majadiliano lengo kuboresha mfumo wa haki nchini.


Rais Samia amesema Serikali katika kuinua maisha ya wananchi hususani vijana, imeendelea kutengeneza ajira katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, utalii na kutoa ujuzi.

Naye Rais Mstaafu wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amesema utawala wa sheria umeleta umoja na uongozi bora kwa nchi za Afrika.

Japo amesema yapo mambo yanaendelea katika mataifa ya Nigeria, Burkinafaso na Congo ambayo yanaacha maswali kuliko majibu.

Amesema zipo mbinu zinazotumika kudidimiza demokrasia kwa nchi za Afrika ikiwemo vyombo vya dola kuwakamata na kuwakandamiza viongozi wa upinzani.