Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia afanya uteuzi, Ulanga bosi mpya ATCL

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Peter Ulanga

Muktasari:

  • Ulanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Peter Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Ulanga anachukua nafasi ya Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.

Ulanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Aidha, amemteua Profesa Harun Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Kabla ya uteuzi huu, Profesa Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe, anachukua nafasi ya Profesa Shadrack Mwakalila aliyemaliza muda wake.

Uteuzi huo ulioanza Novemba 9, 2024 taarifa yake imetolewa leo Novemba 11, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga.