Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia awabadilisha tena Chande, Ulanga

Muktasari:

 Zikiwa zimepita siku mbili tangu Rais Samia Suluhu Hassan afanye uteuzi na utenguzi uliomgusa aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Peter Ulanga leo amepangua tena akimrejesha katika nafasi yake.


Dar es Salaam. Zikiwa zimepita siku mbili tangu Rais Samia Suluhu Hassan afanye uteuzi na utenguzi uliomgusa aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Peter Ulanga leo amepangua tena akimrejesha katika nafasi yake.

Katika mabadiliko ya Septemba 23, 2023 Rais Samia alitengua uteuzi wa Ulanga na kueleza kuwa atapangiwa nafasi nyingine huku kiti chake kikichukuliwa na Maharage Chade aliyehamishwa kutoka kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Leo Jumatatu Septemba 25, Rais Samia amemteua Chande kuwa Postamasta wa Shirika la Posta Tanzania kuchukua nafasi ya Macrice Mbondo ambaye taarifa ya Ikulu inaeleza kuwa atapangiwa kazi nyingine.

“(Rais) amemteua Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Chande anachukua nafasi ya Macrice Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Kwa mujibu wa taarifa ya mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia ameteua Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), John Ulanga kuwa Balozi.

Taarifa ilieleza hatua ya Rais kuivunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) na kumteua Balozi Meja Jenerali mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala huo.

Uteuzi huo umeelezwa kuanza mara moja na Balozi Mteule Ulanga ataapishwa tarehe 26 Septemba, 2023 Ikulu, Dar es Salaam.