Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia afanya uteuzi, uhamisho wa wakuu wa mikoa

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassani amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa mikoa mitatu ya Shinyanga, Tanga na Songwe.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili Februari 26, 2023 Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka imeeleza kuwa wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa ni Christina Mndeme ambae anakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Aidha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Michael nae ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe,

Hata hivyo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amehamishiwa Mkoa wa Tanga, huku aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Omary Mgumba uteuzi wake ukitenguliwa.

Katika uteuzi huyo Christina Mndeme anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ambae alichaguliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.